PASAKA WETU
Kumekuwa na Sikukuu nyingi za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali Duniani kila mwaka, kila taifa Duniani huwa na siku yake maalum ya kukumbuka uhuru wake, ama tukio lolote muhimu kuliko yote. Vivyo hivyo, Mungu naye ameteua siku yake ambayo aliamuru Dunia nzima ishehekee na kufurahia Uhuru na Ukombozi wa mwanadamu. Hii sio siku nyingine, ni siku ya PASAKA. Pasaka ni nafsi, ni uhai, ni mateso ya mmoja kwa ajili ya Ukombozi wa mwingine. Kutoka 12:21 [21] Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka.
Isaka alikuwa na Pasaka wake. Mwanzo 22:13 [13] Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Wayahudi walikuwa na Pasaka yao. Yohana 2:13 [13] Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
Na sisi kama Ulimwengu, hakika tuna PASAKA WETU. 1 Wakorintho 5:7 [7] Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza