Oparesheni Khartoum
Oparesheni Khartoum 01
Misheni Khartoum 01 (Kufa Ama Kupona) Kachero Othuman Seyunguson kutoka nchini Tanzania, anatumwa kweny misheni ya kuinusuru ikulu ya taita la Sudan ambayo ilikuwa inanyemelewa na wadhalimu. Misheni hii iliyopewa jina la Misheni Khartoum 01, haikuwa misheni ya kitoto. Ni misheni iliyojaa usaliti wa kila aina, lakini zaidi adui mkubwa wa taifa hilo la Sudan, Brigedia Omar Al - Bashir alikuwa amejipanga kwelikweli na alihitaji ikulu ya taifa hilo la Sudan kufa ama kupona. Kachero Seyunguson akiwa pamoja na msaidizi wake, Farida mwanadada kutoka chini Kenya, aliyepikwa akapikika kwenye mambo ya mapambano ni kana kwamba walitolewa sadaka kwenye misheni hii maana kila waliyekutana naye mbele yao hata yule waliyedhani yupo upande wao, alikuwa ni adui. Je, nini itakuwa hatima ya wawili hawa kwenye misheni hii iliyojaa visa na mikasa ya kuburudisha, kuelimisha na kukuacha kinywa wazi? Ungana na Mwandishi Abubakar A. Nkundwason, katika riwaya hii ya aina yake.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza