OMBAOMBA ALIYEUZA WANAE
Akiwa ameanza kuuona mwanga kwenye maisha yake, Modester anapata ulemavu unaotokana na wivu wa mapenzi, ambapo pia mpenziwe anauawa kikatili naye anaishia kuwa Ombaomba katika mitaa ya Kariakoo.\r\nAkiwa anaishi mitaani, jua na mvua vikimuishia utosini Modester anakutana na matukio ya kutisha mno,likiwemo la kubakwa na kupachikiwa ujauzito mwingine. inafika hatua anakata shauri na kuamua kuwauza wanae!
Hilo ni suala lililomtafuna katika sehemu kubwa ya maisha yake, mpaka alipokutana na mwandishi wa habari maarufu James Masika \'Masika The Best\', ambaye naye alikuwa kwenye masaibu yake, baada ya mkewe kufungwa jela akikabiliwa na kesi ya mauaji.
Ni Masika aliyekubali kwenda kwenye safari ya \'kifo\' kuwatafuta watoto wa Modester, ombaomba aliyeuza wanae!
NAKUKARIBISHA KATIKA RIWAYA HII YA KUSISIMUA, KUBURUDISHA NA KUELIMISHA.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza