
NYOTA YA MAFANIKIO NA KIBALI
Nyota ya mfanikio ni siri kubwa katika ulimwengu wa roho ambapo watu wengi watumishi wa Mungu hawajui, watu wa giza ndio wanazungumzia sana mambo ya nyota
NYOTA YA MWANADAMU YAWEZA,
1. Kuibiwa
2. Kufunikwa au 3.Kufungwa.
1. KUIBIWA NYOTA.
“ Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa wote wamenaswaika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye rudisha ” Isaya 42:22
Neno hili linatumia lugha ya ajabu sana, linasema watu hawa, inamaana wanaonekana, tunaishinao, tunasalinao, tunaombanao na tunafanyanao huduma lakini wameibiwa. Kiuhalisia mtu aliyeibiwa huwa anafichwa sehemu na kulindwa ili asitoke lakini huyu yeye ameibiwa ila yeye anaonekana. Ameibiwa nini? Mambo ya rohoni. Mtu huwa hastuki sana ukigusa mambo ya rohoni maana mwanadamu anaishi mwilini kwa asilimia kubwa kwa mfano mtuu ukimweleza kuwa mwanao amefukuzwa kazi, anastuka sana lakini ukimweleza kuwa mwanao ameibiwa nyota, anashangaa na anaona jambo la kawaida, kumbe ni bora tatizo la kimwili maana lenyewe sio la kudumu kuliko tatizo la kiroho maana lenyewe ni la kudumu. Mtu akifukuzwa kazi ana matumaini ya kupata kazi nyingine ila akiibiwa nyota yake, ameharibiwa maisha yake kabisa. Inamaana kama ni kazi, hatapata nyingine, kama ni biashara ndio amekuwa maskini hata kama ana mali atashangaa zinaishaje wala hatakuwa na majibu. Hata akipata kazi nyingine ataishia hasara na kisha kufilisika kabisa au kufukuzwa kila anakokwenda
DALILI ZA MTU ALIYEIBIWA NYOTA YAKE,
{i} Kukosa kibali ghafla,
{ii} Hali ya kukata tamaa inakuwa ya kawaida kwake, {iii} Mawazo yanaongezeka sana,
{iv} Kupata magonjwa yanayoshika sana na hayaponi kirahisi,
{v} Matumizi yasiyokuwa ya lazima huongezeka,
{vi} Kama anasali, anajaa Roho mtakatifu kwa muda kisha anaondoka.
{i} Kukosa kibali ghafra.
Mtu aliyeibiwa nyota yake anapoteza pia kibali kama ni mfanyabiashara, hawezi kupata wateja tena, kama ni mwanafunzi anachukiwa ghafra na baadhi ya waalimu na wanafunzi wenzake, kama ni mwanasiasa, anaanza hadi kuzomewa majukwaani, kama ni binti au kijana anatafuta mchumba, atatafuta sana bila mafanikio na kama ni mwana ndoa, ndoa inakuwa na migogoro mingi na inakuwa kwenye hatihati ya kuvunjika kila siku.
{ii} Hali ya kukata tamaa inakuwa ya kawaida kwake.
Nyota ya mtu ikiibiwa, mtu huyu anakata tamaa hata kama anafanya biasharaanaweza kukwambia … “ Unavyoona hivi, mimi nitaacha biashara ” anaweza pia kuacha kazi ofisini wengine hufikia mpaka kuchukua hatua mbaya ya kujiua kwa sababu daima anaona kushindwa tu katika kila analofanya, na jamii unakuta haimuelewi.
USHUHUDA na 1:
Nilikutana na dada mmja alikuwa anaishi maisha ya shida sana hata chakula ni cha shida mume wake alikuwa na studio ya kurekodi miziki yenye mtaji wa milioni 50, ikaungua moto, alikuwa anafanya kazi Tanroad akajisikia tu kuacha kazi ili akae nyumbani ile kaziyake akaenda kumkabidhi rafiki yake. Maisha yake yakaharibika akawa na migogoro isiyoisha kwenye ndoa yake, wakati nakutana naye alikuwa amekata tamaa kabisa. Shida kubwa ya familia ya dada huyu ni kwamba nyota yake na nyota ya mume wake zilikuwa zimechukuliwa ndicho kilichopelekea miradi yao yote kusambaratika na maisha yao kuharibika kabisa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza