
NYOTA ELIMU ILIYOUTEKA ULIMWENGU
Elimu kuhusu nyota ni elimu kongwe zaidi katika historia ila kwa wengi imeanza kusahaulika, elimu hii haifundishwi shuleni/vyuoni kwa upana mkubwa hivyo hupelekea maswali mengi yanayokosa majibu siku hadi siku. Wengi wameitumia elimu hii vibaya kwa kuwadanganya mamilioni ya watu kukiamini kile walichokikusudia wao wenyewe. Ni ajabu sana kama tukikaa kimya pasipo kuangazia ukweli wa kila jambo linalotutatiza.
Katika kitabu hichi utakwenda kujifunza mambo mbalimbali kuhusu nyota, utapata kufahamu chanzo halisi cha elimu hii na uamshwaji wa kiteknolojia uliochochewa kwa chunguzi zilizofanywa na watu maarufu wenye ubobezi wa elimu hii ya nyota.
Katika Maandiko Matakatifu tumejifunza mambo mbalimbali kuhusu uumbaji. Wengi wetu tunamuamini Mungu kama Muumbaji wa Ulimwengu, ila kuna baadhi wameenda mbali kutumia matokeo ya kilichoumbwa kama Mbadala wa muumbaji mwenyewe, hivyo tutakwenda kuangazia kila mahali kuhusu kile wanachokiamini na uhalisia uliopo ambao unatokana na matokeo ya kifikra.
Katika kitabu hiki utakwenda kufahamu dadisi mbalimbali zilizofanyika kama tujuavyo udadisi ni sifa ya kipekee aliyoumbwa nayo binadamu ambayo imepelekea ufanyikaji wa mambo makubwa zaidi na ambayo hayakutegemewa kama yatakuja kufanyika. Sasa chanzo cha dadisi hizo ni matokeo ya kuwepo kwa nyota tunazoziona angani kila usiku.
Ushawahi kusikia habari za kusafisha nyota? Kuibiwa nyota? au pengine ushawahi kwenda kupata huduma hizo mahali fulani? au pengine wewe ni mfuatiliaji mkubwa wa magazeti yanayochapisha habari za ijue nyota yako? Katika kitabu hichi tumeangazia kila sehemu kuhusu mafundisho hayo, chanzo chake na utimilifu wake, utabaki mdomo wazi na kushangazwa katika kujua ni nani yuko nyuma ya mambo haya yote?
Nikukaribishe katika usomaji wa kitabu hiki.
Usomaji Mwema.
Mwandishi
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza