NJIA SABA ZA KUITEKA DAR ES SALAAM
Ukiiteka Dar es salaam utakuwa umeiteka Tanzania.
Dar es salaam jiji lenye ushawishi sana nchini Tanzania na Africa kwa ujumla likitajwa kuwa pia miongoni mwa majiji saba yanayokua kwa kasi duniani kote.
Ni jiji linalobeba sura ya Tanzania kimataifa huku pia likiwa kitovu cha uchumi wa Tanzania takribani17%ya pato la taifa.
Jiji hilo ni fahari ya Tanzania na kilele cha mafanikio ya watanzanja wengi hasa vijana ambao huvutiwa na mtindo wa maisha na fursa nyingi zinazopatikana jijini humo.
Lakini ili kufanikisha kuteka au kushawishi jiji hilo lazima uwe na njia zenye uhakika ambazo zitakuwezesha kuteka jiji hilo.
Kitabu hiki basi kinakuonesha maeneo na mambo Saba ambayo uyatumie ili kujipatia nguvu, jina na ushawishi katika jiji hilo kwenye nyanja uliyopo.
Pia kinaonesha kwa mfano maeneo na njia ambazo watu wenye majina na ushawishi katika nyanja mbalimbali jijini humo na nchini Tanzania wametumia kufika hapo walipo.
Wewe pia una nafasi hiyo na fursa hiyo basi kisome kitabu hiki kwa utulivu fanyia kazi eneo lako au njia yako hakika utakuwa mmoja ya watu ambao wana nguvu katika Tanzania.
Enenda na ufanikiwe.
egsiyaga
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza