NITATIMIZA NDOTO YANGU
Pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wenye ndoto hapa duniani hali halisi inaonesha kuwa ni asilimia ndogo sana ya watu ambao hutimiza ndoto zao. Marehemu Myles Mnuroe aliwahi kusema kuwa watu wengi wanakufa na uwezo wao (bila kutimiza ndoto zao) na kwamba makaburini ndiko sehemu utakapowakuta wakurugenzi wengi waliokufa na makampuni yao ambayo hayakuwahi kuanzishwa. Makaburini ndiko sehemu pekee utakutana na vipaji vingi ambavyo havikuwahi kutumika. Kitabu hiki kinaeleza jinsi unavyoweza kufikia ndoto yako haijalishi. Kitabu kimesaidia watu wengi kuishi ndoto zao.
Les Brown
mzungumzaji mkubwa kule Marekani aliwahi kusema kuwa ili utimize ndoto yako
unahitaji kuwa na njaa ya kuitimiza (you need to be hunger) maana mtu mwenye
njaa hatulii anatafuta kitu chochote cha kupoza njaa yake. Kama una ndoto
lakini huna msukumo wa kuifikia hakika hautaweza kufika pale unapotamani
kufika.Ndoto uliyonayo inabidi ikuendeshe(usitulie).
“Nitatimiza Ndoto Yangu”