
Nini Cha Kufanya Unapotaka Kurejesha Nafasi,mamlaka Na Heshima Uliyopoteza?
Nafasi na Mamlaka yeyote ile lazima ibebe sauti,nguvu,na hata heshima ya kiwango kinachostahili,ingawa wakati mwingine inaweza kuwa tofauti,na hii ndiyo sababu ya makala ya kitabu hiki kuwepo mikononi mwako ili kuhakikisha mamlaka ambayo Mungu amekupa iendane na sauti,nguvu,heshima na utukufu wa ngazi inayostahili.
Tunavyo jadili hoja ya kupoteza nafasi,mamlaka na heshima maana yake ni kule kupoteza au kupungua kwa sauti,nguvu,hadhi,staha na utukufu unaostahili kulingana na mamlaka ya ngazi ya ki utawala uliyonayo au unayo stahili kuwa nayo.
Pamoja na kwamba andiko la kitabu hiki limejijenga na kujikita kwenye kujifunza juu ya kurejesha nafasi,mamlaka na heshima iliyopotea,kama agenda kuu lakini pia utajifunza juu ya;
- Mahusiano yaliyopo kati ya mamlaka,heshima na sheria.
- Viashiria na dalili za kuangalia ili kung'amua kama umepoteza heshima na mamlaka unayostahili.
- Agenda za kujifunza na kuzisimamia ili kukuwezesha utumie vizuri mamlaka uliyonayo itakayokufanya uishi kwenye nafasi yako na heshima ya kiwango unachostahili.
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; (Wafilipi 1:6) |
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza