Nifanye Nini Niwe Ibrahim Wa Vizazi Vyangu
Siri kumi zilizoleta baraka na mafanikio katika maisha ya ibrahim
Ibrahim alitokea katika familia iliyokuwa ikiabudu miungu,lakini pia uwezo wao kiuchumi ulikuwa wa kawaida sana.
Ibrahim alipoitwa na Mungu alikubali wito ,na huo ulikuwa mwanzo wa kubadili historia yake ,ya familia yake na vizazi vilivyofuata baada yake. Ibrahim alibarikiwa na kufanikiwa sana kiasi kwamba baraka nyingine zilizotamkwa juu yake zilivinufaisha vizazi vilivyofuata.
Nilifuatilia historia yake niligundua kuna siri zilizoleta baraka na mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
Yawezekana historia yako na familia yako ni mbaya sana kiasi kwamba huna tumaini ndani yako la kubadili historia hiyo. Lakini nina ujasiri wa kusema siri zile kumi zilozoleta baraka na mafanikio kwa ibrahim zinaweza kuleta na kwako pia.
Kama utajidhatiti kuzisoma na kuziweka siri hizi kumi katika matendo uwe na uhakika historia yako na ya vizazi vijavyo itabadilika.
Hivyo kitabu hiki ni kwa ajili ya ambao wa kiu ya kubadili hiatoria zao,za familia zao na za vizazi vyao.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza