Nguzo 12 Za Uanafunzi
Namna ya Kuibua Thamani Ndani yako kupitia Mafunzo
Taifa lolote linalotaka kupata maendeleo ni lazima liweke kipaombele katika kujenga rasilimali watu bora sana ambo watatumika kuijenga nchi. Elimu ndio nguzo muhimu sana kwa taifa ili kupata watu bora.
Familia, jamii na hata watu binafsi wamekuwa wakijibidiisha katika kutafuta elimu na kufikia ngazi za juu sana lakini bado changamoto kubwa ni wahitimu hao kutokuajirika. Kuna watu wengi sana majumbani na mtaani kwetu pamoja na kusoma bado hawana ajira.
Hali hii ni kwa sababu wamesoma lakini wanakosa kuzijua Siri au Nguzo Muhimu sana katika kujipatia elimu.
Waandishi Adv. Isaack na Daniel Zake wanakufunilia Nguzo 12 muhimu za Uanafunzi katika ngazi yoyote ambazo ukizifuata zinaweza kukupatia nafasi yoyote unayohitaji ili kutoa mchango wako kwa jamii kitaaluma.
Waandishi wanaamini kupitia falsafa ndani ya kitabu hiki utagundua ya kuwa tatizo si ukosefu wa ajira ila watu bora na wenye uwezo wa kutatua matatizo ya jamii ndio wanakosekana.
Kitabu hiki ni mahsusi kwa wanafunzi ngazi ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu, waalimu, wazazi au walezi na watu wote wenye nia ya kuleta mabadiliko juu ya mfumo wa kujifunza katika mataifa yetu ya Afrika.
Pata nakala yako kwa kuendelea kujifunza zaidi
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza