NGUVU YA MAAMUZI Maamuzi Yako Hatima Yako
Ukisoma kitabu hiki kwa umakini, uwe na uhakika maisha yako yatachukua mwelekeo wa mpya wa mafanikio.
Hatima ya maisha ya mtu ni matokeo ya matendo yake, matendo yake ni matokeo ya maamuzi yake, na maamuzi yake ni matokeo ya fikra zake.
Fikra za mtu zinaweza kuboreshwa na kukuzwa, unaweza kuboresha na kukuza fikra zako kwa kupata maarifa sahihi, kitabu hiki kinayo maarifa sahihi ya ki-ungu na kutosha kuboresha na kukuza fikra zako.
Maisha ya mtu ni matokeo ya maamuzi ambayo amekuwa akifanya. Hauwezi kustawi zaidi ya maamuzi ambayo umekuwa ukifanya na wala hauwezi kukwama zaidi ya maamuzi ambayo umekuwa ukifanya katika maisha yako.
Pitia kitabu hiki, fikra zako zitaboreshwa na kukuzwa, na kukuwezesha kuwa mtu mwenye maamuzi yenye nguvu ya kukufikisha kwenye hatima ambayo, Mungu amekusudia uifikie kwenye maisha yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza