![Biashara & Ujasilimia Mali](https://www.getvalue.co/media/products/nguvu_iliyojificha_katika_msalaba.png)
NGUVU ILIYOJIFICHA KATIKA MSALABA
NGUVU ILIYOJIFICHA KATIKA MSALABA
Kitabu hiki kitakuwa msaada kwa wote wanaopenda kutafakari kwa undani kuhusu mateso na kifo cha Yesu msalabani. Kuna faida za kutafakari kuhusu mateso na kifo cha Yesu rnsalabani. Mtakatifu Teresia wa Avilla anasema ni vigumu mtu yeyote anayetafakari mateso ya Bwana Yesu kuishi na dhambi ya mauti. Au mtu huyo ataacha dhambi au ataacha kuendelea na tafakuri. Vitu hivi viwili, yaani kutafakari mateso ya Yesu na dhambi ya mauti haviwezi kukaa pamoja katika moyo wa mtu. Tunapata wazo la namna hiyohiyo kutoka kwa Origen ambaye anasema: “Dhambi haiwezi kutawala katika roho ambayo inatafakari kifo cha Mkombozi daima.” Naye Mtakatifu Bonaventura anatuambia kuwa, “Yeyote anayependa kukua katika fadhila na neema, anapaswa kutafakari daima mateso ya Yesu. Hakuna zoezi ambalo ni la faida zaidi katika kutakatifuza roho ya mtu kama tafakuri ya mateso ya Yesu Kristo.”
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza