Natamani Kuwa Mjasiriamali: Visa Na Mikasa Ya Wajasiriamali
Price:
5,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
May 28, 2021
Product Views:
2,385
Sample
Katika uzoefu wangu katika kuandaa na kuhudhuria warsha na semina za kijasiriamali nimejadiliana sana na vijana wasomi kuhusiana na mada hii. Katika mjadala wawasilishaji wengi walionyesha hali ya wajasiriamali wengi kukata tamaa. Wengi wao wakiingia katika ujasiriamali wakitaka utajiri wa pupa, lakini wengi huishia kwenye kilio na kusaga meno. Kitabu hiki kitawafunda yeyote anayehitaji kuwa mjasiriamali; awe mtoto, kijana na hata mzee. Hivyo ni kusema kwamba wajasiriamali wanofanikiwa hupitia visa na mikasa lukuki lakini kutumia mikasa hiyo kama fursa hatimaye huonja matunda ya kazi yao.
Yawezekana kitabu hiki ni kidogo sana. Lakini mawazo yake ni mubashara na kuntu. Yamekomaa yote. Ijapokuwa si maungwana mjasiriamali kutamba juu ya kazi aliyofanikisha, nachukua fursa hii kusema kitabu hiki kitapanua wigo wa majasiriamali kujisifia pale
atakapotumia vyema elimu ya kitabu hiki kujiletea maendeleo. Ninatamba kwamba kitabu hiki kina mawazo yaliyowiva vizuri. Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu mawazo haya yamepitia kwenye mikono ya vijana na wasomi waliowadadisi mahiri
wa kazi za kijamii.
Katika uzoefu wangu katika kuandaa na kuhudhuria warsha na semina za kijasiriamali nimejadiliana sana na vijana wasomi kuhusiana na mada hii. Katika mjadala wawasilishaji wengi walionyesha hali ya wajasiriamali wengi kukata tamaa. Wengi wao wakiingia katika
ujasiriamali wakitaka utajiri wa pupa, lakini wengi huishia kwenye
kilio na kusaga meno. Kitabu hiki kitawafunda yeyote anayehitaji kuwa mjasiriamali; awe mtoto, kijana na hata mzee. Hivyo ni kusema kwamba wajasiriamali wanofanikiwa hupitia visa na mikasa lukuki
lakini kutumia mikasa hiyo kama fursa hatimaye huonja matunda ya kazi yao.
Nakukaribisheni tukisome kitabu hiki kusudi tujipatie fikra mpya na uzoefu katika ujasiriamali. Mungu awabarikini sana katika ujasiriamali wenu.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza