NAJUTA KWENDA HONEYMOON
NAJUTA KWENDA HONEYMOON
UTANGULIZI……
Waswahili wanasema simulia sana ila omba yasikukute. Mwenzenu yamenikuta. Yaliyonikuta honeymoon sitakuja kuyasahau. Nilichofanywa milele kitabaki moyoni mwangu.Sitasahau kamwe. Naomba ungana nami kwenye hii simulizi ya kweli kujua lipi ni lipi.
Sehemu ya kwanza.
Tukiwa nyumbani baada ya kutoka kufunga ndoa kanisani, ndugu wa Mume wangu walifanya mambo ambayo sikuyaelewa .Kila nilipoyafikiria nilishindwa kupata majibu.
\" Kwanini ndugu zako wanafanya hivi ? \" Nilimuuliza Sam.
\" Wanafanyaje? \"
\" Aaaah! Inamaana huoni wanachokifanya. \"
\" Ndio sioni! Kama ningeona nisingekuuliza. \"
\" Wananikosea heshima . Muda wote wanaangalia maungo yangu. Nikitembea wanaangalia makalio yangu na kuniteta. \" Nilimwambia.
Ajabu, Sam badala ya kuchukia, alicheka .Tena alicheka kicheko kilichoniacha mdomo wangu.
\" Hivi hili ni jambo la kuchekesha?\" Nilimuuliza.
\" Achana na hayo Judi. Jiandae twende ukumbini.Muda umeenda.\" Aliniambia.
Alinishika mkono na kunipeleka chumbani.
\" Jiandae. Saa moja kamili yatakiwa tuwe ukumbini.\" .
\" Lakini Sam....\"
\" Achana na mambo madogo madogo. Jiandae twende ukumbini.\" Aliniambia.
Nilikuwa mpole.
Niliamua kufanya alichokitaka .Nilioga na kujipodoa.
\" Waoooooo.....umependeza sana Mke wangu.\" Aliniambia .Alinisogelea na kunibusu kwenye paji la uso.
\" Ahsante..\" Nilimjibu.
Tuliongozana kutoka chumbani. Tukiwa kwenye korido tulikutana na Baba yake mdogo. Baada ya kuniona nilivyopendeza ,alijishika kichwa.
\" Eeeeh! wewe ni mzuri.. \" Aliniambia. Alinisogelea na kunizunguka kwa nyuma. Alinishika makalio .
\" Mmmmh ...\" Aliguna.
Kitendo cha kunishika makalio kilinikera. Niligeuka na kutaka kumwambia, lakini kabla sijaongea ,Sam aliongea.
\" Sichaguagi vitu vya ajabu ajabu . Si unaona mzigo .\" Aliongea Sam.
Kauli yake ilimaanisha anaunga mkono kitendo cha baba yake mdogo kunishika makalio.
\" Huyu mwanaume wa ajabu sana. Inamaana kitendo cha Baba yake mdogo kunishika makalio anakiona cha kawaida ?\" Nilijiuliza. Nilimtazama nikiwa na maswali.
\" Nitaongea naye baadae. Kama anaona kawaida nitamueleza hii sio kawaida, ni kunikosea heshima.\" Nilijiambia.
.............................................................
Ukumbini.
Tabia ya ndugu wa Mume wangu kuniangalia na kuniteta iliendelea.
Safari hiii tofauti na nyumbani, walikuwa wakiniteta huku wakioneshana kitu kwenye simu. Ni kama kwenye ile simu kulikuwa na picha yangu. Muda wote waliongea huku wakiniangalia na kuangalia ile simu.
\" Hivi hii ni kawaida?\" Nilimuuliza Sam.
\" Judi acha kuharibu sherehe yako. Kwanza usiniulize vitu visivyokuwa na msingi. Tupo hapa kwa ajili ya Kunywa ,kula na kusherekea.\"
\" Nitasherekeaje wakati mambo hayapo sawa. Ndugu zako wanayateta maungo yangu?\" Nilimwambia.
Badala ya kunijibu, Sam alichukua simu yake na kupiga. Alisimama na kwenda pembeni kidogo. Aliongea kwa sekunde kadhaa kisha akarudi .
.....................................
Sherehe ikiwa inakaribia kuisha,majira ya saa tano usiku, wazazi wa Sam yaani wakwe zangu walikuja kutuaga .Wakiwa wanatuaga waliongea kitu kilichoniacha mdomo wazi.
\" Tunatangulia hotelini..\" Aliongea Mama Mkwe.
\" Mmmh! Kwanini waende hotelini? Kwanini wasiende nyumbani?\" Nilijiuliza. Nilimgeukia Sam na kumuuliza.
\" Wanaenda Hotel gani? \"
\" Legend Hotel.\" Alinijibu
Legend Hotel ni Hotel ambayo tulipanga kufanya fungate letu. Kitendo cha kuniambia wazazi wake wanaenda pale kilinichanganya.Sikuelewa wanaenda kufanya nini.
\" Lakini kwanini waende hotelini? Si wangeenda nyumbani .\"
\" Mmmmh! Judi unagubu sana.\" Aliongea kwa ukali Sam.
Sikutaka kuendelea kumuuzi,niliamua kukaa kimya. Lakini gafla, ndugu zake waliokuwa wananiteta sikuwaona . Niliangaza kila pande, hawakuwepo ukumbini.
\" Ndugu zako wameenda wapi ?\" Nilimuuliza Sam.
\" Wametangulia.\" Alinijibu kifupi.
\" Wametangulia wapi?\"
\" Wametangulia Legend Hotel\" .
\" Eeeh! Na wao wameenda legend Hotel? Lakini kwanini wameenda kule? Kumbuka leo tunaanza Honey moon,na tutaifanyia pale.\"
Hakunijibu kitu.
Kutokunijibu kulimaanisha hayupo tayari kuliongelea swala nililomuuliza. Niliamua kukaa kimya.Sikutaka kumuuzi kwa maswali japo kichwani nilijiuliza sababu ya wao kwenda hotelini. Maana kwenye ile hoteli tulipaswa kwenda wawili tu.Mimi na Sam.
...............................
Majira ya saa sita usiku,Sherehe ukumbini iliisha. Mimi na Sam tuliondoka kuelekea Hotelini.
\" Leo ni usiku wetu wa kwanza, nataka uwe wa kukumbukwa.\"Aliniambia huku akinibusu shavuni. Alipeleka mkono wake Ikulu kwangu.
\" aaaaashiii..taratibu bana...\" Nilimwambia .Nilimtoa mkono wake ikulu .
Nilimsogelea na kumnongoneza. \" Mimi ni wako,subiri tufike.\".
\" Leo…..” Alitamka Sam.
Hakukaa sana alitamka tena.
“ Leo…”
“Leo..”
“ Leo nini?” Nilimuuliza.
Hakunijibu. Alitamka tena.
“ .leo....leo....leo....\" Alitamka mara tatu. Aliniangalia kisha akanibinyia jicho.
\" Kwanini anatamka hivi?\" Nilijiuliza moyoni. Sikupata jibu. Niliamua kupuuzia.
………………..
Tulifika Hotelini.
Alinishusha kwenye gari . Alinibeba juu juu kuelekea chumbani. Njia nzima alinibusu na kunipapasa . Ni kama alikuwa na wazimu.
Tuliingia kwenye chumba tulichoandaliwa. Chumba kilikuwa na giza totoro.Alinilaza kitandani na kuendelea kunibusu .Alinitoa nguo na kuniacha kama nilivyozaliwa.
“ Washa taa kwanza..” Nilimwambia.
\" Hivi ndio safi. \" Aliniambia.
\" mmmmh!\" Niliguna. Giza lilikuwa totoro sana.
\" Tunafanyaje mapenzi kwenye giza hili?\" Nilijiuliza. Moyo wangu haukuridhika ila niliamua kupotezea. Sam alinibusu na kunichombeza.Alinigusa na kunichezea sehemu dhaifu.
“ Aaaa…ai…aaaa….” Nililalamika kila aliponigusa.
Gafla, Mwili ulinisisimka. Nywele zilinisimama. Hofu ilinishika na moyo ulipiga kwa kasi.
\" ndi ... ndi...ndi... \" Moyo ulipiga.
Nilitetemeka kwa woga.
Sifahamu nini kilitokea .Nilikosa amani kabisa.
\" Mbona hivyo ?\" Aliniuliza.
\"Mwenyewe Sielewi. ..\'
\"Mmmmh! Basi Usiogope?\" Aliniambia . Alinishika na kunilaza kitandani. Bila kujali hali yangu aliendelea kunipapasa na kunichombeza.
Akiwa anakilamba kifua changu, ajabu,gafla, ............
NAJUTA KWENDA HONEYMOON -NILICHOFANYIWA SITAKUJA KUSAHAU- 02.
\"Mmmmh! Basi Usiogope?\" Aliniambia . Alinishika na kunilaza kitandani. Bila kujali hali yangu aliendelea kunipapasa na kunichombeza.
Akiwa anakilamba kifua changu, ajabu, gafla alitokea mtu na kumpiga kibao.
“ Paaah! Kilitua shavuni.
“Eeeeh! “ Nilistaajabu.
Kabla hatujafanya lolote, yule mtu aliondoka . Alipotea kwenye giza la mle ndani.Nilijaribu kumtazama kwa umakini sikumuona.
“ Huyu nani? Ameingiaje humu?” Nilimuuliza Sam.
Hakunijibu.
“ Ngoja nikawashe taa.” Nilimwambia.
Nilishuka kitandani. Sam alinidaka mkono.
“ Usiwashe taaa. Naomba tuendeleee.”Aliniambia.
“ Aaaah! yaliyotokea unayaona ya kawaida?”
“ Yaliyotokea yepi? Mbona sikuelewi.” Aliniambia Sam.
“ Kwahiyo unataka kunifanya kichaa . Aliyekupiga kibao hujamuona ?”
“ Kibao! Nani anipige kibao? Humu ndani tupo wawili .Nani atanipiga kibao?.”
“ Usitake kunichanganya Sam.. Nimeshuhudia kwa macho yangu. Kuna mtu ametoka gizani na kukupiga kibao. Naomba nikawashe taa tumtafute. Humu ndani sio salama.”
Sam alikataa. Alikataa katakata. Aliniambia hakuna mtu aliyempiga kibao. Aliniambia uchovu wa harusi umenifanya niwe na mawenge.Aliniambia naona vitu visivyokuwepo.
“ Aaaah!’ Nilistaajabu.Nilimwangalia bila kumuelewa.
“ Inamaana hajamuona?” Nilijiuliza.
“ Hapana. Amemuona. Kama hajamuona anazani kibao kampiga nani?” Nilijiuliza.
“ Lakini kama amemuona kwanini anakataa. Kwanini anasema hajamuona? Kwanini anang’ang’ania tufanye kwenye giza?.” Nilijiuliza. Akili yangu iliamini mtu aliyempiga kibao alikuwa mle ndani, na bila shaka aliingia kabla sisi hatujaenda. Swali la msingi alikuwa nani, na kwanini ampige kibao.
“ Unaniangusha mpenzi wangu. Yaani nakuchombeza wewe umekaa tu. Sio poa kabisa. Jaribu kuonesha ushirikiano.” Aliniambia.
“ Sipo tayari kuendelea . Nahitaji kumjua yule mtu . Ameingiaje humu? Unajua mpaka sasa bado yupo humu .”
“ Daaah! Sikutegemea kama ungekuwa hivi.” Aliniambia. Aliniacha na kujilaza pembeni yangu.
Nilimgeukia.
“ Nipoje?”
“ Una maluwi luwi sana. Akili yako haijatulia. Yaani unaona viti visivyokuwepo.”
“Ninachokuambia sio mawazo yangu. Ni kitu cha kweli. Kimetokea mbele ya macho yetu. Kuna mtu amekupiga kibao. Nahitaji kujua ni nani, na ameingiaje humu? .”
“ Hakuna mtu humu .”
“ Kwahiyo naota?.”
“ Sikiliza Judy. Leo ni usiku wetu wa kwanza. Kugombana na kubishana sio kitu kizuri.Kama kungekuwa na mtu ningepambana naye. Lakini hakuna mtu. Naomba nielewe. Naomba acha kuniuliza maswali na kunibishia.” Aliniambia.
“ Inawezekana ni kweli. Huenda nimeona maluwi luwi.” Nilijiambia.
“ Sawa Love.” Nilimjibu.
Alinishika kichwa na kunibusu shingoni.Nami nilirudisha majibu. Tulianza kupapasana na kugalazana. Niligumia naye aligumia. Gafla, alinitaka nimuache. Nilimuacha.
Alinishika vizuri na kuniweka mkao ambao sikuulewa.
“ Unataka kunifanya nini?”
“ Shiiii…” Alinipa ishara ya kutoongea.
Akiwa anajiandaa kufanya alichotaka, alitokea yule mtu tena. Alisogea hadi kitandani na kumpiga kibao .
“ Paaaaah!” Kilitua shavuni.
Safari hii sikushangaa.Nilimuwahi. Nilimdaka mkono. Niliushika mkono wake bila kuuachia.
Simulizi hii imesajiliwa kwa jina la samwely kisinga. Hairuhusiwa kuchapishwa au kusambazwa bila ruhusa yake. Hatua kali za kisheria zitachulikwa kwa wote watakaokaidi.
NAJUTA KWENDA HONEY MOON- NILICHOFANYIWA SITAKUJA KUSAHAU – 03
Safari hii sikushangaa.Nilimuwahi. Nilimdaka mkono. Niliushika mkono wake bila kuuachia.
“ Wewe nani?’ Nilimuuliza. Nilimtazama kiudadisi. Kutokana na giza , na jinsi alivyojifunika sikufanikiwa kumjua
Aliuvuta mkono wake kwa nguvu.Nilimkwaruza na kucha nikamuachia. Alirudi nyuma na kupotea gizani. Haraka nilishuka kitandani. Sam alinidaka mkono.
“ Unataka kufanya nini?” Aliniuliza.
Swali lake liliniacha kinywa wazi. Nilishindwa kumuelewa ni mtu wa aina gani. Aliongea kama hakuna kilichotokea.
“ Kwanini hukunisaidia nilipomshika?” Nilimuuliza.
“ Kumshika nani?” Aliniuliza.
Macho yangu yalitanuka kwa mshangao. ” Hivi naota au?” Nilijiuliza. Nilijishika mara tatu tatu na kuomba nizinduke . Ukweli haikuwa ndoto. Yalikuwa ni matukio halisi yanatokea.
“ Mbona kucha zako zinadamu?” Aliniuliza.
“ Damu za yule mtu. Nimemkwaruza mkononi.”
“ Acha kuongea habari ambazo hazipo. Nimekuambia hakuna mtu humu ndani. Kwanini haunielewi. Muda wote Mtu, Mtu.” Aliongea kwa ukali .
“ Lakini kwanini tubishane? Kama yupo au hayupo tutajua tukiwasha taaa. Naomba tukawashe taa. Humu ndani hakuna usalama. Kuna mtu anatuchezea.”
“ Unamaana gani kusema hivyo?”
“ Inawezeakana kuna mtu anatuwangia.”
“ Hivi na Elimu yangu unazani naweza kuamini mambo ya kishirikina. Hapa hakuna lolote lile, Ishu ni wewe. Unamatatizo ya kisaikolojia. Unaona vitu ambavyo havipo.” Aliniambia.
……………………………………..
Kwa zaidi ya masaa matatu tulibishana. Sam alishikilia msimamo wake, na Mimi nilishikilia wangu. Sikutaka kukubali hakuna mtu wakati nimemuona. Nilimtaka Sam tukawashe taaa.Alikataa kata kata. Alinishika na kutaka tuendelee kufanya mapenzi.Nilimkatalia.
“ Bila kuwasha taaa hakuna mapenzi .” Nilimwambia.
“ Unaleta dharau! Hivi unajua nimelipa shilingi ngapi kwenu?”
“ Hata ungelipa bilioni. Unalotaka siwezi kukubali. Kama hautaki kuwasha taaa haupati kitu kwangu. Labda unibake.” Nilimwambia. Nilichukua shuka na kujifunika.
“ Siku ya kwanza tu unaninyima haki yangu . Huko mbele itakuwaje?” Aliongea kwa huzuni Sam. Alinisogelea na kunipapasa. Niliutoa mkono wake. Nilimuangalia kwa macho makavu na kumpa msimamo wangu.
“ Nakuwa mstaarabu hautaki . Sasa subiri.” Aliniambia. Alilishika shuka kwa nguvu na kulivuta. Alinivamia na kunikandamiza kitandani. Alinishika miguu na mikono.
“ Si hautaki kwa hiari . Acha nitumie nguvu.” Aliniambia.
Alinitanua miguu .
“ ..hale..luyaaaaaaa….yu make me say…hale..luyaaaaa…….” Wimbo ulisikika. Simu yake iliita. Aliniacha na kuipokea.
“ Hallo…..” Aliongea.
Aligeuka kunitazama kisha akasogea pembeni zaidi. Bila shaka hakutaka nisikie mazungumzo yake.
“ Huyu nani anampigia simu Saa Nane usiku?” Nilijiliuza.
Sekunde kadhaa mbele alikata simu na kurudi kitandani.
“ Samahani judy! Alikuwa lengo langu kukufanyia hivi.” Aliniambia.
Nilimtazama bila kuongea lolote.
“ Siwezi kukulazimisha kufanya mapenzi. Naomba tupumzike. Tutafurahia penzi letu kesho. Muda umeenda saizi.” Aliniambia. Alinisogelea na kunikumbatia. Alichukua shuka kwa mkono mwingine tukajifunika.
“ Akilala usingizi nitaamka. Nitaenda kuwasha Taa. Nitamtafuta mtu aliyekuwa humu ndani.” Niliwaza. Nilitulia tuli. Nilimsubiri apitiwe na usingizi.
……………………………………………
“ ngoooo…ngooo..ngoooo….” Mlango uligongwa.
“ Amkeni tafadhali. Mtalalaje mpaka saa tatu….ngoo..ngoo….” Mlango uligongwa tena.
Kwa shida nilifumbua macho. Nilinyosha mkono pembeni ya kitanda kuchukua simu yangu. Niliitazama saaa, ilikuwa saa tatu asubuhi.
“ Nimefeli! Ilikuwaje nikapitiwa na usingizi.” Niliwaza. Mpango wangu wa kuamka usiku na kuwasha Taa ulifeli.
Niliangaza kushoto na kulia kukitazama chumba. Kilikuwa cha ajabu. Kilikuwa kikubwa na Kitanda kilikuwa kati kati.
“ Hiki chumba cha namna gani?” Nilijiuliza. Nikiwa najiuliza Mlango uliendelea kugongwa.
“ Hausikii mlango ukigongwa?” Aliniuliza Sam. Nilisimama kinyonge nikaenda kuufungua. Alikuwa Mama Mkwe .
“ Mnalalaje hadi Saa Tatu. Wahudumu wameshaandaa chai. Tunawasubiri nyie .” Alituambia.
“ Tupe sekunde kadhaa .” Alijibu Sam.
“ Watu wanaotusubiri ni watu gani? Aaah! Itakuwa ndugu zake. Lakini wote kuja hotelini ndio nini! Hii ni honeymoon au ni nini?” Nilijiuliza Moyoni.
Baada ya maandalizi tuliongozana na Sam mpaka nje. Tuliwakuta ndugu wa Mume wangu wakiwa wamekaa kuzunguka meza. Chakula kilikuwa katikati. Walikuwa wanatusubiri . Tulijumuika nao.
Wakati kila mmoja akijipakulia chakula, Macho yangu yalitua kwenye mikono ya Baba Mdogo. Ilikuwa na michubuko. Ilikuwa imekwaruzwa na kucha.
“ Nimempata .” Nilijisema moyoni. Nilisimama kwenye kiti.