Mwongozo Wa Kuishi Kwa Amani Na Furaha
Mwongozo Wa Kuishi Kwa Amani Na Furaha ni kitabu ambacho kimetoa mbinu mbali mbali za watu ambao wamekata tamaa, maisha yao kukosa maana, huzuni, ukiwa, hasira, na n.k jinsi ya kuanza kujenga mtazamo mpya na chanya juu ya maisha na kuanza kuishi maisha na kuyafurahia siku baada ya siku.
Mwanadamu hajakusudiwa kuishi kwa huzuni tu, balik akusudiwa kuyafurahia na kuyakubali maisha yake. Kama maisha sio huzuni tu, ya nini wewe uendelee kuhuzunika na kuyachukia maisha yako kila kukicha?
Maisha ni kama pande mbili za shilingi. Upande mmoja ni ule unaomaanisha furaha, huku upende wa pili ukimaanisha huzini.
Ikiwa maisha yako yote yatakuwa yanamaanisha huzini tu basi itakuwa ni ishara tosha kuwa kuna shida katika maisha yako.
Kila mtu anapenda kuwa na furaha maishani mwake. Lakini ukweli ni kwamba maisha ni changamoto, hivyo furaha na huzuni bado vitakuwa sehemu ya maisha ili kuashiria kuwa mwanadamu hajakamilika na anaishi ili kuridhihirisha hilo.
Kitabu hiki kimeandikwa ili kukumbusha na kukuonyesha kuwa sio vibaya kujihisi vibaya, ila ni vibaya kutokujihisi vibaya. Kuna faida gani upike chakula halafu usijihisi hamu ya kukila?
Kuna faida gani kuyaishi maisha unayoyachukia?
Kupitia kitabu hiki utajifunza njia sita (6) muhimu kabisa kama muongozo wa kukusaidia kujiponya kutoka kwenye huzini na upweke unaokufanya uyaone maisha yako hayana maana kabisa na kupelekea kutaka kujiua au kujidhuru kimwili na kihisia.
Ikiwa kwa muda sasa umekuwa ukiishi kwa kuyachukia maisha yako na kuvichukia vitu na watu wanaokuzunguka, basi kitabu hiki ulichokishika mkononi au kukisoma kwenye kifaa chako chochote cha kidijitali basi jua umeshika tiba ambayo umekuwa ukiitaji na kuitafuta kwa muda mrefu ili kujitibu kifikra, kihisia, kiroho, na kimwili.
Endelea kusoma zaidi...
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza