MWONGOZO WA KUFAULU DARASANI
Nilipotumia kanuni hizi 2003 kwenye matokeo ya mtihani wa taifa darasa la saba iliniwezesha kuwa mtu wa pili katika wilaya .Nilipotumia mbinu hizi mwaka 2007 nikiwa kidato cha nne pale sekondari ya Kantalamba iliyoko Sumbawanga zilinifanya kuwa mwanafunzi bora darasani na matokeo ya mwisho nikapata daraja la kwanza(Division one) na nikafanikiwa kuchaguliwa katika shule ya sekondari ya Pugu ambayo ina historia kubwa ya kutoa viongozi wakubwa wa nchi na baadaye nikajiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam ambacho ni moja ya vyuo vikuu bora katika bara la Africa
Shule unayosoma haiwezi kukufanya wewe ufeli mtihani. Kufeli
au kufaulu hakutegemei wewe unasoma shule gani, unatoka familia gani au kabila
gani bali inategemea juhudi za mwanafunzi binafsi.