Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Mwongozo Katika Mafanikio1 - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO

0.4
3
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 08, 2020
Product Views:
5,793
In category:
Sample

Kila mmoja ana tafsiri tofauti kuhusu mafanikio na wengine wameenda mbali kwa kutafsiri mafanikio kwa namna wao wanavyoona wengine wanasema,lakini mafanikio ni nini? je ni kuwa na hela nyingi? Ni kuwa na familia bora ambayo ina mchango katika maisha yako? Mafanikio ni nini haswa? Twende pamoja katika kitabu cha MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO kupata ukweli huu wa maana halisi ya Mafanikio na namna ya kuyapata.

Kutokana na uchunguzi ambao ulifanyika na chuo cha Strayer
University kilichopo U.S.A-Washington Dc kuhusu kuuliza nini maana
ya mafanikio matokeo yao yalikuja kwa kuonesha kwamba 99% ya
Waamerika wanatafsiri mafanikio kama mtu kitimiza malengo yake na
kuwa na mahusiano mazuri na familia yake pamoja na marafiki zake,
na 34% ya Wa-Amerika ya watu wazima walisema kwamba utajiri ni
kitu muhimu kwao ikiwa ndiyo tafsiri yao ya mafanikio. Wakaenda
mbali katika uchunguzi wao na kuweka tamati kwa kusema kwamba
Asilimia kubwa ya Wa-Amerika wanaamini ishara ya mtu mwenye
mafanikio ni yule mwenye familia imara na yenye msaada kwake.
Mafanikio unaweza kuyatafsiri katika sehemu hizi ;


1.Uchumi wako binafsi.
2. Afya Yako.
3. Mahusiano Yako.
4. Mwonekano Wako Katika Jamii.
5. Umaarufu kutokana na unachokifanya.
6. Cheo Ulichonacho n.k


Tafsiri yako ya mafanikio haiwezi kuwa tafsiri ya kila mmoja katika
maisha yake ndio maana kuna zaidi ya maelfu ya watu waliofanikiwa
ambao kila mmoja ana maana yake ya mafanikio kutokana na hizo
sehemu ambazo nimeweza kukutajia. Kwa kuwa watu wengi tunaona
mafanikio katika upande wa kiuchumi (Fedha), vyeo na kuamini
ndizo zenye maana yenyewe halisi,kiasi kwamba maana ya mafanikio
kwa upande mwingine imekuwa ikididimizwa na kushusha wengine
ambao wapo upande mwingine kabisa ya maana ya mafanikio. Nataka
nikusihi tuu kwamba NDIYO ya mwaka 1993 na miaka mingine ya
nyuma inaweza kuwa NDIO kwa mwaka huo lakini kwa mwaka 2018
na kuendelea ikawa ni HAPANA kubwa sana kwahiyo usikaririshe
maisha kwa maana unayoijua ya mafanikio.


Inawezekana unaona kama wewe huwezi kuwa mjasiriamali kutokana na majaribu na changamoto ambazo umepitia kwa kipindi cha nyuma
cha kujaribu kuwa mjasiriamali, inawezekana upo kwenye ajira na
unaona kuwa na mafanikio ni ndoto, inawezekana ni mwanafunzi
unaona huna muda wa kuweza kujenga ndoto yako, inawezekana
pia huna elimu ya darasani ukadhani kwamba maisha yako lazima
yaishie pabaya,inawezekana pia umetoka katika familia yenye
mazingira magumu na mbele yako unaona ndoto yako ya kuwa
mfanyabiashara imekufa kabisaa, inawezekana pia hujui umuhimu wa
mitandao na jinsi ya kuongeza watu katika mtandao wako n.k Lakini
kumbe inawezekana Mafanikio yako yapo sehemu ingine tofauti na
inawezekana pia mafanikio yapo hapo hapo katika kitu unachokifanya
sema tuu kwasababu umekosa mwongozo bora ndio maana unaona
huna unalolifanya katika maisha yako.


Kitabu hiki cha MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO ni kitabu
ambacho kimelenga sehemu zote kukuongoza kukupa matokeo mazuri
ya maana halisi ya mafanikio yako bila kukutenga au kukuondoa nje
na mtizamo wako wa mafanikio. Kitabu hiki kimebeba majibu ya
maswali mengi ambayo umekuwa ukijiuliza na kujitia wasiwasi ndio
maana tumekiita MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO kwasababu
kama kweli utakuwa umejitoa katika kufanya yale ambayo utayakuta
katika kitabu hiki jua tayari utakuwa umeshaweka msingi wako wa
mafanikio na kitakachobaki ni wewe kuendelea na ujenzi wako kwa
kujitoa na kuwa na imani kwamba mwisho utafika na utadumu zaidi
katika vizazi na vizazi.

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold