Mwanachuo Diary: Namna Unavyoweza Kufanikiwa Kimaisha Kuanzia Chuoni
Namna Unavyoweza Kufanikiwa Kimaisha kuanzia Chuoni
Ndani ya kitabu hiki kuna Funguo za Kukusaidia wewe Mwanachuo, Uweze kujua ni kwa Namna gani Unaweza Kufanikiwa Kimaisha kuanzia Chuoni, hata kama Umechaguliwa kwenye Chuo Usichokipenda au Kozi uliyoambiwa HAINA SOKO.
Haijalishi uko Mwaka wa Kwanza, Mwaka wa Pili, Mwaka wa Tatu, Mwaka wa Nne, au Mwaka wa Tano [ikiwa unasomea Udaktari]... kitabu hiki kinakufaa sana.
Haijalishi Changamoto uliyonayo. Iwe ni ya Kielimu, Kimahusiano, Kifedha, Kiroho, au Kitabia... kitabu hiki kinakufaa sana, na tena kitakupatia hatua rahisi za kukutoa hapo ulipokwama kwenda kule unakokutamani.
.
Hiki kitabu kimeandikwa kwa ajili yako. Ukiwa unakisoma, unaweza ukadhani kulikuwa kuna Mpelelezi aliyekuwa akiyafuatilia Maisha yako na kuja kuyaweka Hadharani; kwa sababu kimesheni zaidi ya 90% ya Maswali yaliyokuwa yanakusumbua kwa muda mrefu.
Kwa upande mwingine, Kitabu hiki Kitakusaidia kujua namna unavyoweza ku_balance mambo ya chuoni na mambo yako binafsi; Ili uweze kunufaika Chuoni na Mtaani.
Kama Hakitakusaidia kama ulivyoahidiwa, basi una haki ya kuomba kurejeshewa Pesa yako.
WAKATI NI SASA. JICHUKULIE HIKI KITABU SASA HIVI. USISEME UTAJICHUKULIA BAADAE AU KESHO.
Kwa kadiri unavyopoteza Muda, ndivyo unavyojichelewesha kuyafikia Mafanikio yako yanayoanzia papo hapo ulipo. Na Kwa kadiri unavyopoteza Muda, ndivyo GHARAMA YA KITABU INAVYOPANDA. Usishangae kurudi na kukikuta kinauzwa Tsh. 20,000/=
KUMBUKA: Hiki kitabu kina kurasa 127+ Zilizoshiba, na KIMEKWISHA KUWASAIDIA WATU WENGI WALIYOKUWA NA HALI MBAYA ZAIDI YAKO.
AHADI YETU KWAKO: Endapo utajipatia kitabu hiki ndani ya Saa 24 za Leo, basi utapata na Zawadi nyingine ya kitabu cha Bure kabisa, kitakachoendelea kukunoa zaidi. (Kitabu chenye Thamani ya shilingi 5000+), pamoja na USHAURI wa BURE juu ya Ndoto zako za kimaisha (kwa Wiki moja).
BOFYA KITUFE CHA \"BUY NOW\" HAPO JUU - KUJIPATIA KITABU CHAKO SAHIVI
KUHUSU MWANDISHI
Lackson Tungaraza ni Mjasiriamali, Mwamasishaji, Mhubiri, Mwanzilishi wa Lamax Quotes na Lamax Designs, na Mwandishi wa Vitabu kadhaa ikiwa ni pamoja na kile kiitwacho ‘SITARUDI NYUMA TENA’ ambacho kilianza kusambazwa nchini Oktoba 2017.
Kwa jinsi mbali mbali Mungu amekuwa akimtumia kusema na watu wake. Ameandika masomo mbali mbali na Kuwafundisha Vijana kweli ya Neno la Mungu huko Mitaani, Makanisani na Vyuoni, hasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma aliposomea Shahada ya kwanza ya Uhandisi wa programu za kompyuta (Bachelor of Science in Software Engineering) katika Ndaki ya Mawasiliano na Elimu Angavu (CIVE).
Mwaka 2017 Alikuwa akifundisha Masomo ya Ujasiriamali ICE FM Redio ya Njombe katika Kipindi cha ‘Bodaboda Chukua Utulivu’ cha kila Alhamis asubuhi, na Mwaka 2018 kuandikwa katika gazeti za ‘THE CITIZEN’ kutokana na Mchango wake katika tasnia ya Uandishi wa vitabu.