Muongozo Wa Maombi Ya Uchumba
Muongozo Wa Maombi Ya Uchumba
Kumekuwa na mlipuko wa mahusiano ya uchumba kuvunjika katika jamii zetu, vijana wanaishi katika hofu kubwa sana kutokana na kupoteza tumaini katika mahusiano yao ya uchumba. Kumekuwa na kuchumbia na kuachana, kumekuwa na mahusiano ya mtu kuwa na wachumba wengi kwa wakati mmoja, hii ni dalili kubwa sana kwamba kunatatizo kwenye eneo la mahusiano ya uchumba kwa vijana. Kitabu hiki ni jibu la changamoto ya mahusiano ya uchumba kwa vijana na kwa watu wengine waliopo kwenye mahusiano ya uchumba. Kimebeba miongozo ya maombi ya kuombea mahusiano wakati wa uchumba, namna ya kuanza maombi na namna ya kumaliza, maandiko ya kusimamia wakati wa maombi ya kuombea mahusiano ya uchumba, sababu za kwanini tuombee mahusiano wakati wa uchumba, n.k