MTU MPYA
Wakati tunajifunza habari za mtu wa kwanza hapo juu bila shaka ulizifurahia sana, nafikiri ulitamani tuendelee kutafakari habari za mtu huyo ambaye alikuwa mwakilishi wa Mungu hapa duniani, ambaye kila kitu kilitetemeka sauti yake ilipozungumza, hata wanyama walioko baharini, nchi kavu na walioko chini ya ardhi walipoisikia sauti yake walipaswa kutulia kumsikia Kiongozi wao anasema nini, walitamani kumsikia akiwapa maagizo ya kiutawala ambayo aliyapata kutoka katika kikao ambacho alikifanya jioni na Muumba wa vyote.Nafikiri habari za mtu huyo zilikufurahisha sana oooh! Hata mimi zilinifurahisha nakumbuka wakati mwingine nilipokuwa nazitafakari nilimtazama mke wangu na kusema wewe haukuwa mtu wa kawaida niliwaza namna ambavyo tungedumu milele na mpenzi wangu huku tukiyafurahia maisha milele wala kifo kisingetutenganisha, niliwaza namna ambavyo ningewaona wajukuu wa wajukuu wangu, niliwaza namna ambavyo tungekuwa na upendo wa ajabu, niliwaza namna ambavyo kusingekuwa na chembe hata moja ya huzuni duniani, kila wakati tungekuwa watu wa kufurahi tu.Shetani hakufurahia kabisa namna ambavyo Mungu alimuumba mtu wa kwanza, kiufupi shetani alimuonea kijicho au wivu mtu wa kwanza namna ambavyo alikuwa kiumbe wa ajabu sana, namna alivyokuwa na uwezo mkubwa kutawala dunia, namna alivyoongoza wanyama na kuwapangia majukumu yao ya kila siku. Kwa muda mrefu shetani alitafuta mbinu za kumwangusha mtu huyu wa kwanza ili apoteze utu wake halisi duniani yaani apoteze heshima aliyokuwa nayo kwa wanyama na viumbe hai vyote, alikuwa akitamani kumfuata Adamu ili amdanganye lakini hakuweza kwa namna ambavyo Adamu alikuwa jitu la kutisha kamwe shetani asingeweza kusimama mbele yake kirahisi na kuongea udanganyifu. Adamu duniani alikuwa akimuwakilisha Mungu yeye alikuwa zaidi ya malaika, kama Mungu aliamua kutuma malaika duniani aliwaamuru na kuwaambia nendeni duniani mkamsikilize Adamu atakachowaambia fanyeni., hivyo walipofika duniani walikuwa wanakuja kwa mwakilishi wa Mungu duniani ambaye huwa anafanya kikao na Mungu mara kwa mara. Hivyo shetani alipaswa kwenda kwa mtu wa kwanza kwa tahadhari kubwa vinginevyo angepewa adhabu kali.Waebrania 1:14 Je! Hao wote sio roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?Mtu wa kwanza alikuwa ni mwakilishi wa Mungu na hivyo malaika wote waliokuja duniani walikuwa wakimuheshimu yeye kama kiongozi wa dunia hii, Mungu alimvika fahari kubwa sana mtu kiasi kwamba shetani alikuwa haelewi kwanini Mungu ameamua kufanya jambo kubwa kiasi hicho, hata mtunga Zaburi nae alipokuwa anatafakari alishangaa sana.Zaburi 8:4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu, umemvika taji ya utukufu na heshima.Umesoma vizuri hiyo mistari miwili ya mtu ikionyesha namna ambavyo mtunga zaburi anashanga na kujiuliza mtu ni kitu gani? Anajiuliza kwanini Mungu aliamua kumvika utukufu mkubwa kiasi hiki? Amemfanya mdogo punde kuliko Mungu maana yake nafasi yake iko karibu sana na Mungu. Jambo hilo lilimsumbua shetani na aliamua kumshawishi mtu wa kwanza atende dhambi na kwa kweli halikuwa jambo la kawaida kwa shetani kumdanganya Eva, mimi nafikiri hata alipokuwa akiongea uongo wake hakumsogelea alikaa mbali mno na kama ulifuatilia maongezi ya shetani na Eva ni kuwa utaona shetani alikuwa akiongea kwa kutetemeka na hofu kuu, kwa sababu alijua alikua akiongea na Mungu wa dunia hii hivyo anaweza akaingia kwenye hatia kubwa na kupata adhabu kali kutoka kwa Mtu wa kwanza ikiwa atagundulika ni muongo, hivyo aina ya uongeaji wa shetani ilikuwa ni kama vile mtu amepata habari fulani ya umbea hivyo anakuja kumueleza mtu.Mwanzo 3:1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?Umesoma vizuri huo mstari kama ukirudia zaidi ya mara moja utagundua kuwa shetani hakuwa na ujasiri wa moja kwa moja kusimama mbele ya mtu hivyo alijaribu kujifanya amepata habari mahali fulani na kumletea Eva.Jambo la kusikitisha sana ni kuwa watu wa kwanza walikubaliana na wazo potofu la shetani na hapo kukatokea msiba na huzuni kubwa duniani na mbinguni ambayo haijawahi kutokea. Mtu wa kwanza mara tu alipotenda dhambi alipoteza utu wake au uungu ulokuwa ndani yake, kitendo hicho cha kupoteza uungu ndani yake kilimpotezea sifa ya kuwa mtawala wa dunia hii, hivyo kilimtoa kwenye nafasi yake ya kiutawala na kumuondolea mamlaka lakini pia kilimuondolea haki ya umilikiMwanzo 3:9-10 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi?10 Akasema nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Mfano wa Mungu? Nini ilikuwa maana yake?Yaani awe na Uungu ndani yake?Akatawale dunia kama yeye anavyotawala mbinguni?Yaani awe na ufahamu kama wake?Awe na mamlaka kuu duniani?Yaani amiliki kila kitu?Yaani vyote vimtii? Hadi Simba na Chui? Ooohh!!!Yaani asidhurike na kitu chochote, hadi moto ?Majibu ya maswali yote hapo juu ni NDIYO, Mungu aliweka Uungu ndani ya mtu, kama kila kitu kinavyo mtii Mungu na kumuogopa vivyo hivyo vilipaswa kumtii na kumuogopa mtu duniani, mfano Simba, Moto, Upepo, Nyoka, Chui, avitawale vyote na kuvimiliki vyote.Huyu ni mtu ambaye Mungu alimkusudia duniani, Je wewe una sifa kama hizo?Roho mtatakatifu awe ni mwalimu wako katika darasa hili, karibu tujifunze pamoja. Naamini utakuwa MTU MPYA mara baada ya kusoma kitabu hiki.BARIKIWA SANASURA YA 1MTU MPYA DUNIANIPengine umeshangaa kuona neno mtu mpya Duniani! Hata mimi pia nilishangaa sana niliposikia neno hili akilini mwangu, imekuwaje mtu mpya tena? Bila ya kukupotezea muda rafiki yangu nipende kukujulisha kuwa duniani kuna watu wa aina kuu mbili ambao ni mtu mpya na mtu wa zamani. Kwa bahati mbaya sana watu wapya ni wachache mno. Mungu aliamua kumuumba mtu kwa makusudi na sababu zake na sababu yake kuu ilikuwa mtu huyu awe mwakilishi wake duniani katika shughuli za kiutawala. Umewahi kuwa mwakilishi wa mtu fulani katika shughuli fulani? Mfano wewe ni mwalimu mkuu msaidizi halafu kinatokea kikao mkoa fulani na kinamuhitaji mwalimu mkuu, kutokana na majukumu mbalimbali ya huyo mwalimu mkuu anaamua kukuteua wewe uende ukawe mwakilishi wake katika kikao hicho.Utakapoenda kwenye hicho kikao utakuwa ni mwakilishi wa mwalimu mkuu lakini huko utafanya majukumu yote ambayo huyo mwalimu mkuu alipaswa kufanya, utajibu maswali yote ambayo huyo mwalimu mkuu alipaswa kuyafanya, kiufupi utakuwa ni mwalimu mkuu msaidizi kwa jina ila kiutendaji na mamlaka, huko utakuwa ni mwalimu mkuu. Huwezi kutumwa kumwakilisha daktari kwenye kikao ikiwa wewe taaluma yako ni mwalimu, ndiyo huwezi kumwakilisha mkuu wa majeshi ikiwa wewe ni mwanariadha, kwanini huwezi kumuwakilisha mtu ikiwa hamfanani taaluma? Jibu ni rahisi ni kwa sababu hutakuwa na ufahamu au uwezo kama wa yule unayemuwakilisha, hivyo basi ili uweze kumuwakilisha mtu fulani lazima uwe na uwezo unaofanana au kukaribiana na mtu huyo unaye muwakilisha.Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Oooooh! Umenielewa ni kwanini ilibidi Mungu atuumbe kwa mfano wake? Kama nilivyokueleza hapo juu ya kuwa huwezi kuwa daktari na ukaenda kwenye kikao cha marubani kumuwakilsha rubani haiwezekani, kwanini haiwezekani ni kwa sababu hamfanani taaluma?Mungu alituumba ili tuwe wawakilishi wake hapa duniani hivyo kwa sababu aliamua kutuumba ili tuwe wawakilishi wake hivyo ni lazima tufanane naye la sivyo hatuwezi kumuwakilisha. Nilikwambia kuwa ikiwa mwalimu mkuu msaidizi ataenda mahali fulani kumuwakilisha mwalimu mkuu basi atatakiwa kufanya majukumu yote ambayo mwalimu mkuu alitakiwa kuyafanya kama angekuwepo, hivyo uwezo wa mwalimu mkuu msaidizi unapaswa kufanana na mwalimu mkuu huyo au hata ukitofautiana usiwe kwa kiwango kikubwa ambacho kinaweza kusababisha baadhi ya mambo yasikamilike. Hebu twende kuangalia baadhi ya mambo ambayo mtu huyo wa kwanza alikusudiwa kufanana na Mungu.MAMLAKA YA KIUTAWALAKama tulivyojifunza hapo mwanzo ni kuwa mwalimu mkuu anapoamua kumruhusu mwalimu mkuu msaidizi kwenda kwenye kikao fulani kumuwakilisha huwa anampa mamlaka ya ukuu huko aendako maana yake kwa kipindi yupo kwenye kile kikao yeye ni mwalimu mkuu aliyetumwa na mwalimu mkuu pale kuwakilisha ukuu wa yule aliyemtuma. Kiufupi mtu aliumbwa kama Mungu na alipoletwa duniani alikuwa ni Mtu mwenye Uungu ndani yake au aliyebeba Uungu ili kumuwakilisha Mungu mkuu hapa duniani. Mwanadamu alitumwa kuonyesha Uungu hapa duniani.Mithali 8:16 Kwa msaada wa Mungu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.Umesoma vizuri mstari huo wa biblia, kama hutojali unaweza kurudia kusoma tena ili kuongeza nafasi ya kutafakari kwa kina zaidi. Anasema kwa msada wa Mungu wakuu hutawala, wakuu ni watu hivyo tunaweza kusema kwa msaada wa Mungu watu hutawala. Kwanini mpaka msaada wa Mungu ndipo watu watawale? Kwa sababu Mngu ndiye mkuu wa vyote na mwenye mamlaka kuu hivyo huwapa watu mamlaka ya kiutawala. Huwezi kutawala ikiwa huna mamlaka ya kiutawala, ngoja nikupe mfano Je mnaweza kukaa kikao nyumbani kwenu na mkamchagua kaka yenu mkubwa awe askari wa barabarani halafu mkamshonea sare kisha mkamwambia nenda barabarani ukakamate madereva wasio na leseni? Hata kama huyo mtu atavaa sare kama za jeshi la Polisi lazima atakamatwa na kupewa adhabu anapewa adhabu kwa sababu hakuchaguliwa na vyombo vyenye mamlaka hivyo hana mamlaka ya kutawala kama Polisi.Mamlaka ni nguvu isiyoonekana ambayo inampa mtu uwezo wa kihalali wa kumiliki eneo fulani au kufanya majukumu fulani. Mfano Askari wa barabarani anayo mamlaka ya kusimama barabarani na kukagua leseni za madereva na kuvikagua vyombo vyao lakini kamwe daktari hawezi kuamua kwenda barabarani kukagua leseni za watu, unafikiri kwanini hawezi? Je daktari siyo mtu kama askari? Jibu ni rahis wote ni watu lakini wanatofautiana mamlaka na utofauti wao wa kimamlaka unatofautisha au kuonyesha mipaka yao ya kiutawala. Huwezi kulala na kuamka asubuhi halafu ukaamuaa kujitangaza kuwa wewe ni Raisi wa nchi, hata kama wewe ni pacha wa raisi aliyeko madarakani bado huwezi kujitangaza kwa sababu lazima utangazwe na mamlaka husika kuwa wewe ni Raisi wa nchi, utakapotangazwa na hiyo mamlaka ndipo utapokea mamlaka ya kutawala. Ndiyo maana mtu mwenye akili alisema kuwa kwa msaada wa Mungu wakuu hutawala kwa sababu alijua kuwa wakuu ndiyo wenye mamlaka lakini je na wao hizo mamlaka wametoa wapi? Jibu ni kwa Mungu mwenye mamlaka kuliko mtu au kitu chochote.Adamu alitangazwa na Mungu kuwa ni mtawala wa Dunia hii hivyo Adamu alipewa mamlaka na Mungu kumuwakilisha duniani. Ukweli ni kuwa Adamu alikuwa na uwezo mkubwa wa kiutawala hapa duniani kuliko tunavyofikiri na Mungu alitaka watu wote tuwe na mamlaka ya kutawala duniani. Adamu alikuwa na uwezo wa kumuita Simba na simba akisikia sauti yake popote alipo anakimbia haraka sana mpaka kwa Adamu na kumsikiliza anasema nini Bwana mkubwa, Adamu alikuwa na uwezo wa kumwita Tembo na kumtuma akafanye kazi fulani na tembo akatii kwa haraka sana, Adamu alikuwa na uwezo wa kusema neno lolote duniani likatokea, Adamu alikuwa na amri juu ya chochote kile duniani, alikuwa na uwezo wa kumwambia Simba afe na akafa muda huo huo, Adamu hakuwa mtu wa kawaida Miti ilipomuona akitembea ilikuwa ikito salama za heshima kwake, Wanyama wasingeweza kusima mbele ya Adamu wakati anapita kama mtawala walipaswa kusimama, hakuwa mtu wa kuzuiwa na chochote. Adamu alikuwa na uwezo wa kuiamuru mvua inyeshe na ikanyesha lakini pia alikuwa ana uwezo wa kuifunga mvua, Adamu alikuwa na uwezo wa kuihamisha bahari. Adamu alikuwa anajua viumbe wote idadi yao na mahali wanakoishi. Adamu alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kusema chochote kikatokea Duniani. Mbingu na nchi zilikuwa zinamtambua ya kuwa yeye ni mtawala Duniani.Mwanzo 2:19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila myama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.Majina ya viumbe vyote hai Adamu aliyajua na kuyataja huu ni uwezo mkubwa wa ufahamu ambao pia ulidhihirisha uungu ndani ya Adamu kwa sababu ili umuwakilishe mwalimu mkuu lazima ufahamu wako uwe unafanana au hautofautiani sana, Mungu alikuwa anajua maji yote ya viumbe alivyoumba alimletea Adamu ili aone Je anaweza kuwaita majina yao kama mimi. Jambo la ajabu ni kuwa Adamu hakukosea jina hata moja la kiumbe hai, nilikwambia mwanzo kuwa Adamu aliwajua viumbe hai wote, waliokuwa wanaishi kwenye maji, waliokuwa wanaishi juu ya ardhi, waliokuwa wanaishi chini ya ardhi na sio tu kuwajua alikuwa na uwezo wa kuona kiumbe cha chini ya ardhi, alikuwa ana uwezo wa kuona kiumbe hai ndani ya bahari. Ukweli ni kuwa mtu huyu hakuhitaji kusoma kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiakili ndiyo kama aliweza kutaja majina ya wanyama bila kufundishwa unafikiri alihitaji kukaa darasani kufundishwa kuhesabu? Kama alitaja majina ya wanyama unafikiri alishindwa kuyaandika? Unafikiri alitakiwa kujifunza kuongea lugha fulani? Ni kwa sababu tumepoteza uwezo wetu wa akili ndiyo maana tuko hivi.Adamu alikuwa akifikiri kama Mungu hii ni ajabu sana, lakini jambo lililonishangaza ni huo mstari kuwa Adamu alitaja majina yote ya viumbe hai , hivi unafikiri ilichukua muda gani kutaja majina hayo ya hao viumbe? Unaweza ukafikiri ni muda mrefu ni kwa sababu tumepoteza utu wetu wa zamani lakini kwa Adamu ambaye ali
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza