MTAJI ADUI
Hekima ya kumtumia adui kukufikisha kwenye mafanikio yako.
Mtafiti mmoja alifanya utafiti kutaka kujua juu ya mchango wa marafiki na maadui kwenye mchakato mzima wa kufikia mafanikio.
Katika utafiti wake aligundua kwamba watu wengi aliowahoji walimwambia asilimia kubwa ilisababishwa na juhudi za maadui zao kuliko marafiki zao.
Ndio ! Najua utaanza kujifikiria na wewe pia, angalia sehemu nyingi ambazo ulikuwa hauna hamu ya kuendela kupambana kutokana na kero ya watu furani au vitu furani vilikupa hamasa ya kutaka kutoka kwenye kero hizo.
Adui anamchango mkubwa sana kwenye safari yako kuelekea mafanikio kama utamtumia kwa usahihi.
Leo nataka nikufundishe kwenye kitabu hiki kwamba si wakati wote unapaswa kulaani uwepo wa Adui kwenye maisha yako wakati mwingine ndio watu wanaotufanya na kutulazimisha kuona mambo tuliyozani hayawezekani kwa sababu yao yakawezekana.
Ni hekima kubwa kutambua kwamba adui zako wana kwenye mchakato wa mafanikio yako.
Baadhi ya vitu utakavyojifunza kwenye kitabu Cha MTAJI ADUI.
1:: *Maana ya ndani zaidi ya adui.*
2:: *Mtazamo wa adui (Nini anawaza adui)*
3::*Kwanini wakati mwingine hata waliojuu yako au walikuzidi vitu fulani bado na wao wanakupiga vita?*
4::*Kwanini marafiki zako wanaweza kugeuka maadui zako wa kwanza*
5::*Namna ya kumtengeneza adui awe daraja la kufikia mafanikio yako*
6::*Ni maamuzi yako adui awe tatizo au fursa (namna ya kumfanya adui awe fursa)*
7::*Jifunze kuhusu sura ya upande wa neema wa tatizo*
8::*Zijue aina za maadui hatari zaidi kwenye maisha Yako*
9::*Namna ya kumgundua adui yeyote anayewinda maisha Yako*
10::*Kwanini unachukiwa?*
11::*Namna ya kumtumia adui kuinuka na kung'ara zaidi*
12:: *Hekima ya kumshughurikia adui*
13::*Ufahamu juu ya hazina aliyoibeba adui Kwa ajili yako*
Na mengine mengi utayapata kwenye kitabu hiki .