Msamaha Ni Tiba Ya Majeraha Ya Nafsi
\"TANGAZA MSAMAHA UIPONYE NAFSI YAKO\"
Kusamehe ni tabia ya Mungu wetu na kama baba yetu alivyo imetupasa na sisi tuwe kama baba na tufanye sawasawa na baba yetu. Hakuna namna unaweza kusamehe kama Mungu hakai ndani yako ama hufanyi apendavyo Mungu.
Ukweli ni kwamba Mungu alitangulia kutupenda na kutuonyesha huruma kupitia mwanaye wa pekee hivyo hata sisi kwa njia ya kristo tunawezakuwahurumia na kuwasamehe wengine. Sio swala la kujitahidi bali kwa sababu yeye ni anakaa ndani yetu tunayafanya yale ayafanyayo baba yetu. Nje ya Yesu Kristo hakuna msamaha hivyo basi Yesu anapopata nafasi ndani yako uwezo wa kusamehe unajengeka ndani yako. Tunasamehe wengine kama na Kristo alivyotusamehe sisi.
Kusamehe ni huduma kama huduma zingine, vile ulivyohitaji huruma na msamaha wa dhambi kwa Mungu ndivyo unavyopaswa kuwahurumia na kuwasamehe wengine. Kristo Yesu ndiye mfano wetu katika hili tabia hii ya Kristo inapozaliwa ndani yetu hatutatumia nguvu nyingi kusamehe bali hutokea dhahiri.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza