MLANGO WA KUINGIA KWENYE AJIRA
Hatua za mafanikio katika soko la ajira: mwongozo wa kuwafikia waajiri na kuwa na kazi yenye furaha.
Ajira za sasa zimekuwa ngumu na za kugombania. Kila kukicha mifumo ya kuajiri wafanyakazi inabadilika na kukatisha tamaa wasaka ajira. Watu wamefanywa kuwa watumwa kwenye suala la Kupata kazi, kila kona wasomi wanatembea na bahasha kusaka kazi, wanatoa hongo (rushwa) za kila aina na wanapanga foleni kugombania kazi hivyo hivyo kwa wasiosoma lakini ajira kwao bado ni kitendawili kisicho na jawabu. Msomi hana thamani ndani ya jamii kwa sababu anazidi kupoteza muda kutafuta kazi bila ya kutatua changamoto zinazomkabili na zinazoikabili jamii yake na kuifanya elimu aliyoipata kuwa huduma kwa jamii na kuwa chanzo cha kipato kwake. Makosa makubwa anayoyafanya msaka ajira ni kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira pasipo na utambuzi sahihi na uelewa wa soko la ajira jinsi lilivyo na njia gani zitamsaidia kupata kazi kiurahisi. Msaka ajira kama anahitaji kupata kazi kiurahisi kitabu hiki ndiyo mwongozo bora wa kumsaidia mlango wa kuingia kwenye mfumo wa ajira na kumfanya mmiliki wa cheki namba na kumjengea heshima kubwa. Mtu yeyote anayepambana kutafuta kazi kitabu hiki ni dira na msaada mkubwa sana kwake pale atakapofuata miongozo iliyomo.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza