Mjue Shetani Wa Mahusiano Yako
Tunaishi katika zama na kizazi ambacho suala la mahusiano na ndoa linaonekana kupoteza sana thamani. Haishangazi kuona ndoa nyingi zikivunjika muda mfupi tu baada ya kufungwa, mahusiano kuvunjika mara kwa mara na vijana wengi kutotaka kuingia kwenye ndoa kabisa. Ni imani yangu kuwa, kitabu hiki kitapunguza ongezeko la 'single mothers' na 'single fathers' kwa kuonesha njia sahihi za kuyafurahia mahusiano na kuyaendesha na kuyafanya mahusiano yako kuwa ya mfano wa kuigwa. TIMIZA MALENGO YA MAHUSIANO YAKO! DUMISHA NDOA YAKO.
*Ukiona watu wanalalamika kipindi mpira udundapo, kwa kiasi kikubwa watu hao hao ndio huwa walioudundisha mpira huo!* Shida ya mahusiano yako au ndoa yako kwa kiasi kibwa wewe unayelalamika ndiye uliyesababisha. Kitabu hiki kinaeleza namna ambavyo unaweza kuutuliza mpira udundao (kutatua matatizo ya mahusiano yako au ndoa yako) na kurudisha tena ile furaha na matumaini mliyokuwa nayo katika mahusiano au ndoa yenu kabla. Kitabu hiki kimeweka wazi sehemu ambazo tafiti na saikolojia ya mahusiano inaonesha watu wengi hukosea bila wao kutambua na kujikuta wamehatarisha mahusiano yao. Pia kitabu hiki kimeeleza namna ambavyo unaweza kuyaepuka makosa hayo na kujenga mahusiano bora kabisa kuwahi kutokea. NAKUTAKIA MAFUNZO MEMA NA MUNGU AKUBARIKI.