MJASIRIAMALI NI MHANGAIKAJI
ZIFAHAMU TABIA ZA MJASILIAMALI ZITAKAZO KUFANYA UFANIKIWE KIMAISHA
Ujasiliamali ni chanzo chako cha kuwa tajiri. Lakini utajiri unakutaka ubadilike ujenge tabia nzuri za kukusaidia kufanya ya msingi ili kupata manufaa makubwa katika shughuli yako.
Kitabu hiki kimebeba ujuzi wa kipekee utakaokusaidia kuzijua fursa zinazokuzunguka na namna ya kuzitumia .
Pia kitabu hiki kimesheheni tabia muhimu ambazo wewe mjasiliamali unatakiwa kuwanazo. Kimeongelea kwaundani sana tabia nyingi zinazomuboresha mjasiliamali. kwa asili ya mjasiliamali anatakiwa kuwa na sifa nyingi zikiwa pamoja na kuwa imara, jasiri, mbunifu na mwenye uelewa mpanaa. Kwa hiyo kitabu hiki kitakufanya utoe maamuzi ya kimafanikio, utajenga tabia ambazo zinanguvu ya kukusogeza mbele mtazamo wako wa akili utabadilika.
Pia utajifunza kuwa kutengeneza baadhi ya bidhaa ni rahisi na hivyo utaufungua moyo wako na akili yako, utahamasika kujifnza kwa vitendo namna ya kutengeneza bidhaa unazozitaka.
Kitabu hiki ni tafiki yako mwenza unayeweza kuongea naye wakati wote. Utaboreka ajabu hautakuwa ulivyokuwa mwanzo kabla ya kusoma Kitabu hiki