
MIUJIZA ISHARA NA AJABU
Kiu yangu kubwa toka siku ya kwanza naanza kujifunza Utumishi ilikuwa ni kutenda miujiza nimewahi kufunga maombi ya miaka minne kila jioni nakula chakula kidogo au matunda Tu, nikimlilia Mungu siku zote anipe nguvu zake miujiza itendeke katika Utumishi wangu. Nakumbuka maono niliyoyaona yaliyopelekea kuandika Kitabu hiki
MAONO 13/11/2013
“Namuona mchungaji Gwajima akiwa kwenye mkutano wa Injili , miujiza mikubwa ikafanyika katika uwanja ule baadaye nikaona watu wengi wamekaa makundi makundi wengine watumishi wakubwa wa Mungu, wakaanza kusema” Hizi ni nguvu za giza, huu ni uchawi kabisa” basi nikasikia sauti ikisema “ unaona hawa wanachokisema? hawa hawamwambii mchungaji maneno haya bali wanamwambia Roho Mtakatifu. Na hawa wote nitawakataa: wafundishe watu wangu habari ya miujiza huku ukiwaonesha na mifano yake, wasiwe wanahukumu pasipo kuongozwa na Roho Mtakatifu”.
Hili ni tatizo kubwa sana katika kizazi chetu hiki kilichojawa na usomi na ustaaarabu mpaka kwenye kazi ya Mungu kikaingiza ujuaji na usela katika kazi ya Mungu.
Namuomba Mungu aibariki kazi hii ya kwanza ya uandishi japo kwa ufupi sana nimejaribu kuelezea kanisa la leo na miujiza, ishara na ajabu.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza