MISINGI 12 YA MAOMBI
Ufahamu juu ya maombi yenye majibu
Moja ya vitu vinavyo wakatisha tamaa watu wengi leo wasiombe ni kwasababu wamekosa majibu juu ya yale waliomwomba Mungu.
Wengi wameona hakuna haja ya kuomba kwasababu hawaoni mabadiliko yoyote.
Moja ya vitu vibaya zaidi vinavyo uwa juhudi za mafanikio kwa haraka ni kukata tamaa , ndugu yangu huna haja ya kukata tamaa katika kitabu hiki nimekuandalia ni kwa namna gani unaweza kuomba na ukapata majibu ya maombi yako.
Usikate tamaa njoo tujifunze pamoja katika kitabu hiki.
Katika kitabu cha Misingi 12 ya maombi haya ndiyo baadhi ya mambo utakayojifunza kitabuni;
1::Utajibiwa swali la kwanini unapaswa kuomba Kwa kina na kupewa umuhimu wa maombi kwako.
2:: Utajifunza maana ya ndani zaidi ya maombi ambayo itakuchochea hamasa ya kuwa muombaji.
3::unawezaje kuomba pasipo kukoma? Utajifunza namna ya kuwa na maombi yasiyo na ukomo.
4::Utajifunza kwanini maombi yako mengi hayajibiwi,
5::Utajifunza nguvu ya kipekee itakayobadilisha maisha Yako inayopatikana kwenye maombi.
6:: utajifunza namna sahihi ya kuomba na kupata majibu ya kile ulichokiomba.
7:: Utajifunza misingi 12 ya maombi ambayo ukiifahamu na kuyajenga maombi yako juu yake hutokuwa mtu wa kawaida.
8:: utajua nguvu ya kila MSINGI na namna unavyoweza kukuletea majibu ya tofauti.
9::utaona umuhimu wa kuwa na kila MSINGI WA MAOMBI kwenye maisha Yako ya kiroho.
10:: utajua namna ya kuinuka Tena na kuwa mtu mwenye nguvu za rohoni.
Na mengine mengi utajifunza kwenye kitabu hiki.