MICHAKATO YA UPANDAJI WA MAKANISA MAPYA
Hiki ni kitabu kinachohusu michakato ya kuanzisha makanisa mapya katika maeneo yote; vijijini na mijini
Changamoto tuliyo nayo siku hizi ni kwamba Watumishi\r\nwengi hawapendi kusikia neno kupanda kanisa kwa sababu wanataka kurithi\r\nmakanisa tu. Ninaposema kurithi kanisa maana yake ni kwamba wanahangaika\r\nkutafuta makanisa ambayo tayari yamekwisha kupandwa na watu wengine nao\r\nwanataka kuwa Wachungaji viongozi au wasaidizi katika makanisa hayo.
Ingawa tunahitaji kupanda makanisa mapya kwa kadri\r\niwezekanavyo, tunahitaji kujiuliza, je tunayo misingi mizuri ya Kibiblia kwa\r\najili ya kazi hii. Ni dhahiri kwamba “upandaji wa makanisa ambao hauwezi\r\nkuzingatia tafakari ya kitheolojia juu ya mambo ya utume ambayo kanisa limepewa\r\nna Mungu ni kujikusanyia idadi ya watu kanisani tu, ambayo ni matayarisho ya\r\nchangamoto za karne ijayo.<!--[if !supportFootnotes]-->[1]<!--[endif]-->
Tunahitaji kujenga uwezo si kwa nadharia\r\npeke yake, bali kwa vitendo kamili. Ni ukweli usiopingika kwamba kipindi cha\r\nmtume Paulo alipokuwa akipanda makanisa ni tofauti sana na kipindi cha leo.\r\nWakati wa akina Paulo hapakuwa na compyuta, hapakuwa na simu, hapakuwa na\r\nmagari kama tunayotumia leo, hapakuwepo na bodaboda/pikipiki. Lakini jambo moja\r\nmuhimu sana ambalo linaweza kutufanya tufuate nyayo zao; watu bado ni wale\r\nwale. Hapana mabadiliko yoyote kwa watu. Mzungu na Mwafrika ni walewale tofauti\r\nni mahali tu wanapoishi. Kwa hiyo wanadamu hawana tofauti sana. Tofauti walizo\r\nnazo zinasababishwa na mazingira tu lakini ndani ya mioyo yao bado wako vile\r\nvile. Kama ni kutenda dhambi kila mmoja anatenda dhambi. “wote wamefanya dhambi\r\nna kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Rum. 3:23)
Hivyo basi kitabu hiki kinaweza kuwafaa Wachungaji,\r\nWainjilisti pamoja na Watumishi wengine wanaoitwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kupanda\r\nmakanisa.