
Michakato Na Harakati Za Nyuma Ya Pazia
Ninapoandika juu ya michakato ya nyuma ya pazia ninaandika juu ya milolongo, sheria, kanuni, taratibu, itifaki, mbinu na hata hatua zinazofanyika na kupitiwa nyuma ya pazia ili kutengeneza jambo au alama fulani ambayo imekusudiwa kufikiwa.Waswahili wanamsemo wao,"ukiona vyaelea ujue vimeundwa”.Msemo huu unaweza kuwa na maana nyingi lakini ninayoiona mimi zaidi ni kutuonyesha kuwa nyuma ya vinavyopendeza kuna vilivyo unda na visivyo onekana na wakati mwingine hata havipendezi vikionekana lakini ndiyo kiini na siri ya uzuri unao onekana.Ni kusudio langu na maombi yangu kwa Mungu juu ya kitabu hiki, kikuongezee maarifa ambayo yatabadilisha kesho yako kwa kushughulikia vitu ambavyo pengine ni vigumu sana kuvipa umuhimu wakati ndivyo ambavyo vitakusaidia kusogea mahali pazuri zaidi.
Yapo mambo yasiyodhahiri kwa wengi lakini ndiyo yamebeba,asili,kiini ,siri na kufanya kuonekana kama yalivyo.Ukweli utabaki kwamba kuna mambo yasiyo onekana,yasiyojulikana,yasiyo zungumzwa na pengine yasiyo eleweka wala kuthaminiwa hata kama yatazungumzwa,ambayo kimsingi ndiyo kiini na nguvu ya matokeo tunayoyaona.
Dhumuni hasa la kitabu hiki ni kukuongezea maarifa yatakayo kusaidia kupiga hatua kwa ufasaha. Hasa kwa kutoa mkazo kwenye maeneo na mifumo ambayo haionekani kwa namna inavyostahili lakini ndiyo inayobeba mafanikio ya kila hatua unayokabiliana nayo.
Ndani ya kitabu hiki,utajifunza kwa upana mambo yafuatayo.
- Siri na nguvu ya nyuma ya pazia.
- Heshima ya nyuma ya pazia.
- Nafasi ya ulimwengu wa Roho nyuma ya pazia.
- Mambo ya msingi ya kufanya nyuma ya pazia
- Mifano halisi ya ndani na nje ya biblia na namna inavyoweza kukusaidia kuongeza ustadi,ubora na ufanisi.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza