Mfuko Wa Dharura
MFUKO WA DHARURA\\\\r\\\\nMara nyingi watu wakiwa katika neema wanasahau kabisa kuhusu changamoto. Wakiwa katika kazi wanazo zipenda na kuwalipa vizuri wanasahau kuwa kuna kufukuzwa kazi. Wakiwa kwenye mahusiano mazuri wanasahau kama kuna siku maradhi yataingia katikati yao. Vile vile watu wenye biashara zinazofanya vizuri wanasahau kuwa kuna siku biashara zao zitayumba na kufilisika kabisa. \\\\r\\\\nMaisha ya binadamu yana pande mbili, furaha na huzuni. Kila unapokuwa katika furaha, unapaswa kujiandaa kupambana na machungu ya huzuni itakapokufikia. Ukiwa unasherekea harusi kwa furaha ili hali jirani yako anasafirisha mwili wa aliyekuwa mke wake mpenzi kwenda kumzika, jiandae kwa hilo pia. Kama nyumba ya mfanya biashara mwenzako inatangazwa kupigwa mnada kwa kushindwa kulipa mkopo, wala usimcheke na kudhani hakuwa makini katika biashara. Hayo ni mapito ambayo siku nyingine utayapita.\\\\r\\\\nDharura ni kitu ambacho hakikwepeki wala kuzuilika. Kila mtu anatakiwa kujiandaa na dharura yake. Unatakiwa kuandaa mwavuli kabla mvua haijaanza kunyesha. Maandalizi ya kupambana na dharura pindi ikitokea yatakusaidia kuendelea kutimiza malengo yako hata kama dharura ikikufika.\\\\r\\\\nMara nyingi dharura zinazotokea huwa zina hitaji fedha ili kuzitatua. Ili kuwa katika nafasi ya kutatua changamoto hizo, unatakiwa kuwa na pesa ya kutosha. Hapa ndipo mfuko wa dharura unapokuja. Unatakiwa kuwa na mfuko wa dharura ambao utakusaidia kuhimili changamoto za kipindi kigumu. Mfuko huu utakusaidia kuhimili kipindi umefukuzwa kazi, nyumba yako imeungua, umeuguliwa na mwanafamilia ama biashara yako imefilisika.\\\\r\\\\nWatu wengi huwa wanaongeza matatizo pindi wanapopatwa na matatizo kwa kuwa hawafanyi maandalizi mapema. Mtu anaweza kuwa na tatizo linalohitaji shilingi laki tano kulitatua, kwa kuwa hana pesa hiyo anajikuta anaingia kwenye madeni yasiyo kwisha ili kuweza kutatua tatizo huzika. \\\\r\\\\nUtafiti uliofanywa na gazeti la Money Magazine umebainisha kuwa 78% ya watu wote ulimwenguni watapatwa na majanga makubwa yasiyotarajiwa ndani ya miaka kumi. Utafiti unaongelea majanga hayo yaweza kuwa ni kufukuzwa kazi, kupata ajali, kuunguliwa nyumba, biashara kufa, kupata changamoto ya kiafya na kukosa uwezo wa kufanya kazi. Asilimia hizi ni kubwa sana ambapo kila walipo watu mia moja, watu 78 wanatarajiwa kupata changamoto kubwa ndani ya miaka kumi.\\\\r\\\\nUtafiti mwingine ulifanywa na bodi ya magavana wa Federal Reserve System nchini Marekani mwaka 2018, kuhusu uwezo wa kiuchumi wa familia za wamarekani. Utafiti ulifanywa kuchunguza ikiwa familia hizi zitakosa chanzo chochote cha kipato zitaweza kuishi kwa kipindi gani kwa kutumia akiba zao? Utafiti huu ulifanywa kwa familia 12,000 na kugundua kwamba 60% (ambapo ni familia 7,200) ya familia hizi zilikuwa hazina akiba ya kuwasaidia kuishi walau kwa mwezi mmoja. Ripoti ikaendelea kuwa, 17% (ambapo ni familia 2,040) ya familia zote, zina pesa ya akiba kujikimu kwa miezi chini ya sita, wakati 23% (ambapo ni familia 2,760) tu ya familia zote ndio wenye uwezo wa akiba ya kujikimu kwa miezi sita .\\\\r\\\\nMajibu ya utafiti huu yana maanisha kuwa, 77% ya wamarekani hawawezi kuishi kwa miezi sita bila kuwa na kipato kinachoingia. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirika kwenye kipindi cha kufungiwa kwa shughuri za kiuchumi kutokana na maamukizi ya virusi vya COVID-19 ambapo familia nyingi sana ambazo zilikuwa zinategemea kipato kutokana na mishahara kimeshindwa kuendelea kujikimu japo kwa mwezi mmoja. \\\\r\\\\nNchini marekani magari mengi ya kifahari yamepanga foleni yenye urefu wa kilomita moja na nusu kwenda kwenye kituo cha msaada kwa ajili ya kupewa chakula cha msaada kutokana na mlipuko wa virusi vya COVID-19. Ukiachana na madhara ya ya kiuchumi ya virusi hivi, kutokuwa na mfuko dharura ndio uliofanya watu washindwe kujikimu japo kwa mwezi mmoja. Kupangana kuomba chakula cha msaada ni ushahidi tosha kuwa watu wengi hawaweki akiba kwa ajili ya kipindi cha dharura.\\\\r\\\\nKatika hali ya kawaida, haiwezekani mtu uwe una miliki benzi au BMW mpya halafu uwe kwenye foleni ya kupewa chakula cha msaada ambapo hata mwezi haujaisha toka usimamishwe kazi. Suala ya kufunga biashara na ofisi kama mkakati wa kupunguza maambukizi ya virusi vya COVID-19 ingefanywa na serikali ya Tanzania, hali ingekuwa mbaya zaidi. Watu wengi hawana utaratibu wa kuwa na mfuko wa dharura.\\\\r\\\\nUtafiti mwingine uliofanywa na Federal Reserve kuangalia ni jinsi gani wananchi wapo tayari kipindi majanga yakiwatokea. Waliwauliza watu ikiwa wamepatwa na tatizo linalohitaji dola 400 (ambazo ni sawa na shilingi 920,000) wangetoa wapi pesa kutatua changamoto hiyo? Majibu yalionyesha kuwa, 63% ya wamarekani wanaweza kutoa kiasi hicho kwenye akiba zao na 37% watahitaji mikopo au msaada ili kutatua tatizo hilo. Nchi iliyoendelea kama marekani ina asilimia hizo za watu wanaoweza kulipia janga kutoka kwenye akiba zao, vipi kwa nchi kama Tanzania? Hali si mbaya sana?\\\\r\\\\nUkifikwa na dharura mtu pekee wa kupambana nayo ni wewe. Kila mtu ana mambo yake ya kufaya. Wapo wachache watakao kusikiliza japo hawata kusaidia. Wapo wengine ambao watakusikiliza na kukusimulia dharura zao ambazo ni kubwa kuliko yako. Wapo pia watu watakao kusikiliza na kisha kwenda pembeni kukucheka. Mtu sahihi kutatua changamoto hizo ni wewe. Andaa uwezo wa kutatua changamoto zako sasa. Andaa mfuko wa dharura. Mfuko wa dharura unaandaliwa kipindi ambacho hauna dharura. Andaa mfuko wa dharura sasa!
Utafiti uliofanywa na gazeti la Money Magazine, Asilimia 78 ya watu wote duniani wanatarajiwa kupata majanga makubwa ndani ya miaka kuni. Majanga hayo ni pamoja na kufukuzwa kazi, biashara kufilisika, kupata ajali, kupoteza mali kubwa ama kupata maradhi yatakayo wafanya walale kitandani kwa muda mrefu.
Watu wengi wanapata changamoto kila majanga yakitokea, wanakosa pesa kwa ajili ya kutatua changamoto hizo. kitu ambacho kinapelekea kuingia kwenye changamoto zingine kama za madeni.
Mfuko wa dharura ni kitabu ambacho kitakusaidia kupambana na changamoto zote zitakazo kutokea bila kuhangaika kutafuta mikopo na misaada.
Ni kitabu ambacho kitakupa muongozo wa kuishi maisha yasiyo na msongo wa mawazo.