Mduara Wa Dhambi
Kwamba huitaki dhambi fulani lakini bado unaifanya, na kwa kadiri unavyojitahidi kuiacha dhambi hiyo ndivyo dhambi mpya zinaibuka na kukung’ang’ania.rnrnFikiria dhambi kama shimo kubwa lenye utelezi, ukishadumbukia humo huwezi kujitoa mwenyewe. Utajitahidi kutoka lakini utarudi chini tena, na utaendelea kuchafuka. Kinachofuata, unakata tamaa kuacha dhambi na kuona utakatifu na usafi ni jambo lisilowezekana
Mbaya zaidi matokeo ya dhambi ni dhahiri mno, hayajifichi. Mtu anaweza kuifanya dhambi kwa kificho, watu wasimwone lakini hataweza kuyaficha matokeo ya dhambi aliyoifanya.
Unafanyaje sasa?
Kwenye kitabu hiki nimeeleza jambo moja la kufanya ili upate mgeuko wenye uelekeo wa kuishinda dhambi na kisha kuishi maisha ya utakatifu na usafi. Si hivyo tu, kupata mgeuko huu kunaambatana na kurejeshwa kwa nafasi uliyokuwa umeipoteza kwa sababu ya dhambi, na kuyajua mambo gani uanze kuyafanya katika upya ambao umeupokea.
Amua kutoka kwenye mduara wa dhambi!.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza