Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Mbinu Za Kupata Mtoto Mwenye Afya Bora1 - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

MBINU ZA KUPATA MTOTO MWENYE AFYA BORA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
3,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Dec 14, 2024
Product Views:
76
In category:
Sample

Jipatie kitabu kinachozungumzia mbinu kadhaa za kupata mtoto mwenye afya bora.

   Kila familia duniani hutamani kupata watoto watakaokuwa na manufaa kwao kwa siku za usoni kama wazazi, jamii na kwa taifa lao kwa ujumla.Watoto wenye afya nzuri kimwili, kiakili, kijamii, kiroho na kimaadili.Lakini pamoja na tamaa hiyo hawafanyi maandalizi sahihi ya kufanya njozi yao itimie.Matokeo yake wanapata watoto tofauti na matazamio yao wenye afya duni, wenye tabia mbaya na badala ya kuonekana kama baraka kwa wazazi wao,  jamii au taifa, wanaonekana mzigo na laana.Haiwezekani kupata mtoto mwenye afya bora bila kufanya maandalizi maana hata mkulima ili aweze kuvuna mavuno mengi katika eneo dogo lazima aweke sawa ardhi ya eneo hilo analolilima kwanza.

   Maandalizi ya kupata mtoto mwenye afya bora yanafanyika kabla ya kufunga ndoa(kabla ya kuoa au kuolewa), kabla mama hajashika mimba.Tena yanatokana na afya bora ya wazazi wote wawili(baba na mama) na mama akiwa ndiye kiwanda anayemtunza mtoto huyo akiwa tumboni miezi tisa.

   Kitabu hiki unachokisoma sasa kimejaa mbinu kadhaa za kukuwezesha kama mwanandoa kupata mtoto mwenye afya nzuri kimwili, kiakili, kijamii, kiroho na kimaadili. Kimejaribu kubainisha sababu kadhaa ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kupata mtoto mwenye afya mbaya katika nyanja mbalimbali za maisha kabla ya kuoa au kuolewa, kabla mama kupata ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kuzaliwa mtoto.

   Kitabu hiki ni matokeo ya mafundisho ya afya niliyowahi kufundisha kwenye mikutano ya kanisa iliyofanyika mwaka 2015, Jimbo la Magharibi mwa Tanzania.Kitabu hiki ni zawadi kwa vijana, wachumba na wanandoa karne ya 21.Nakutakia mafanikio na baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu unapoendelea kupokea zawadi hii ya maarifa kwa kusoma na kujifunza mashauri na kanuni zilizomo katika kitabu hiki.

Maranatha! Bwana wetu Yesu Anakuja

Lubango L Chikanda

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold