MATTERS OF THE BLOOD
MATTERS OF THE BLOOD. Yajue mambo yahusuyo DAMU (Laana na Baraka za Familia)
Mafanikio yoyote katika maisha ya Mwanadamu iwe ameokoka au hajaokoka yanahusiana kwa kiasi kikubwa sana na ushirikiano wa damu alionao mtu na familia yake au ukoo wake.
Wapo watu ambao pamoja na kuokoka bado wanaishi maisha ambayo yanafanana kabisa na ndugu zao wengine katika familia au ukoo wao. Wapo watu ambao pamoja na kuokoka bado wanateseka na magonjwa ya kifamilia, shida, mikosi na roho fatilizi za kifamilia.
Neno la Mungu linasema; “Ewe Yerusalemu! Mtu akitaka kutumia methali juu yako atasema: \'Kama mama alivyo ndivyo alivyo binti yake.\" (Ezekieli 16:44).
Hii inaonyesha kuwa inawezekana kabisa alipokwama, kushindwa au kuanguka mama yako au baba yako na wewe ukakwama na kuanguka hapohapo.
Damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani ilimwagika kwa makusudi kabisa ya kutuokoa sisi kutoka katika miunganiko ya damu ya familia zetu na koo zetu ambazo kwa namna moja au nyingine zimekuwa kizuizi chetu kikubwa katika kufikia mafanikio na makusudi ya Mungu maishani mwetu.
Neno la Mungu linasema;
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” (2Kor 5:17)
Kitabu hiki kitakufungua macho na kukufundisha namna ambavyo muunganiko wa damu katika familia yako unaweza kuathiri maisha yako, lakini utajifunza kwa upana zaidi somo la Laana na hasa Laana za familia ambazo zimekuwa zikiwatesa watu wengi.
Muhimu zaidi kitabu hiki kimeambatana na Maombi ambayo yatakuongoza na kukusaidia hata kwa mtu asiyejua kuomba kabisa kutoka katika vifungo vya familia vinavyosababishwa na muunganiko wa damu na maombi ya kujitoa katika Laana na kujiambatanisha na baraka ya Mungu.
Kitabu hiki kitayabadilisha maisha yako na kukupa mwanzo mpya katika safari yako ya Wokovu. Mungu akubariki
JIPATIE NAKALA NYINGINE KUTOKA KWA PASTOR TONY OSBORN
MUONGOZO WA MAOMBI YA KUFUNGUA MWAKA NA BARAKA ZA KILA MWEZI https://www.getvalue.co/prod/muongozo_wa_maombi_ya_kufungua_mwaka_na_baraka_za_kila_mwezi
SILAHA ZA VITA VYETU https://www.getvalue.co/prod/silaha_za_vita_vyetu
KUUWEZA WAKATI UJAO https://www.getvalue.co/prod/kuuweza_wakati_ujao
SIGNS AND TOKENS https://www.getvalue.co/prod/signs_and_tokens
KWAKUA SASA UMEOKOKA https://www.getvalue.co/prod/kwa_kuwa_sasa_umeokoka
NDOTO UANZOOTA NA UHALISIA WAKE https://www.getvalue.co/prod/ndoto_unazoota_na_uhalisia_wake
CHRISTIANS IN THE BUSINESS WORLD https://www.getvalue.co/prod/christian_in_business_world
DEALING WITH ADDICTIONS https://www.getvalue.co/prod/dealing_with_addictions
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza