MATOKEO 6 HATARI YA ZINAA KWA MWANADAMU
Ungojwa hatari unaoleta maangamizo makubwa na hatari sana katika maisha ya MWANADAMU ni Dhambi ya zinaa.Mathayo 12:39, Yesu anakiita kizazi cha zinaa ni kizazi kibaya sana, ni kutokana na MATOKEO yake yanavyoleta madhara makubwa kwa mwanadamu.Hiki kitabu kimekuja kufungua macho ya watu wote kutambua, Dhambi ya zinaa.Inavyo tafuna maisha yao ya kila siku na kizazi chao chote. Kijana ukitaka ufike kwenye kusudi la maisha yako leo ambayo Mungu amekukusudia ; basi tambua madhara ya zinaa.Jambo la kujua leo zinaa, ndio silaha hatari ya shetani kumfanya mtu kutoka \\\" Hero to zero ndio silaha pekee ambayo shetani anaitumia juu ya MWANADAMU, Ili aangamize maisha ya MWANADAMU na kizazi chake chote . Kwa kusoma hiki kitabu kitakusaidia utambue matokeo hatari utakayo pata kama ukifanya zinaa.
Hiki kitabu na imani ,kitawasaidia watu wengi hasa vijana ambao ndio walengwa wakubwa yaliyoko nyuma yake.
Kama ukisoma kitabu hiki , kitakusaidia kutoka katika utumwa wa roho za zinaa, na pia kitakusaindia kukulinda na hatari kubwa sita anazo pata mwanadamu pale anapo fanya zinaa.
Pia tambua kuna aina mbali mbali mtu anaweza fanya zinaa bila yeye kujua ,wala kutambua,sababu shetani anaajenda nyingi za siri za kumtumikisha mwanadamu kwenye zinaa bila yeye kujua , hiki kitabu kimefichuwa aina hizo zote zilizo jificha sirini.
Watu wengi leo awajua chanzo cha matatizo yao ya natokana na nini, ngoja ni kwambie zinaa imeuwa uchumi wa watu wengi, zinaa imepeleka watu wengi kuzimu , zinaa imeharibu ndoa za watu wengi, zinaa imezuia na kuharibu maono na malengo ya watu wengi, hatima nyingi zimezuiliwa sababu ya zinaa.
- Zinaa ndio silaha ya shetani kumfanya mtu kutoka HERO TO ZERO
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza