Mathematics Made Easy
Jenga msingi imara wa hisabati kwa mtoto wako.
Je, mtoto wako ana changamoto katika somo la hisabati? Ungependa mtoto wako wa darasa la tatu amalize mada za darasa la nne bila yeye kufahamu kuwa amemaliza? Unatamani kuona mtoto wako wa darasa la nne anafanya marudio huku akijiandaa na mtihani wa taifa? Najua unapenda sana mtoto wako awe na msingi imara wa hisabati. Kuna wakati unatamani kumpa mazoezi mtoto wako lakini unayakosa? Natambua vile unavyopata shida kumuelekeza mtoto wako awapo na home work. Ulitamani sana upate kitabu chenye mifano inayojieleza ili uitumie kumfundisha mtoto wako. Hivi unajua ugumu wa hisabati kwa watoto mara nyingi husababishwa na ugumu wa vitabu wanavyofundishiwa? Ulikuwa na kiu ya kupata kitabu cha hisabati rahisi ambacho dada na kaka wa mtoto wako wanaweza kukitumia kumfundishia mdogo wao? Kitabu hiki cha MATHEMATICS MADE EASY kimekuja kujibu maswali yote hayo na kurahisisha hisabati kwa mtoto wako kwa gharama nafuu sana.