MAPINDUZI NA MATUMIZI YA AKILI
MAPINDUZI NA MATUMIZI YA AKILI
Utulivu na amani ni muhimu katika kuwezesha maendeleo endelevu, kama ilivyo ghasia ni moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo hayo ili kuyafikia malengo tuliyojiwekea kama nchi au taifa. \r\nNi jambo la kutia moyo kuwa vita na migogoro kati ya nchi na nchi vimepungua, lakini bado utulivu na ghasia ndani ya nchi vimeongezeka na kusababisha vifo na machungu kwa raia. \r\nHali hii ikiendelea suala la kutokomeza umaskini litabakia kuwa ndoto kwa wengi iwapo jamii ya kimataifa haitashirikiana kumaliza migogoro, ukosefu wa utulivu, kuongeza ujumuishi, uongozi bora na maendeleo kwa wote.\r\nDunia hii inawezekana kabisa kuwa sehem salama ya watu kuishi bila vita au ukosefu wa amani, kuishi bila matatizo au shida haiwezekani kwa kuwa shida ni sehem ya maisha yetu ili kuweza kukamilishiana mahitaji yetu.\r\nShida zitokanazo na ukosefu wa mahitaji ya kawaida ya kibinadam, hizi ndizo shida tunazoweza kusema ni sehem ya maisha yetu. Kukosa na kupata ni sehem ya maisha yetu pia, lakini kukosa au kupata kunaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine.\r\nMaana yake ni nini jambo hili, unaweza kukosa kiasi Fulani ya kile ulichokuwa unataka na ukapata kiasi Fulani pia usichokitaka au usichokitegemea.\r\nMatatizo mengi na ukosefu wa amani hapa Duniani, unasababishwa na sisi wenyewe au watangulizi wetu. Ambao wanashika uongozi wa Dunia, au kwa lugha nyingine naweza kusema mataifa yaliyoendelea sana kwenye kila Nyanja hasa kwenye sekta ya uchumi yamejiimalisha sana.\r\nUkosefu wa upendo kwa viongozi wa hizi nchi zilizoendelea kiuchumi, ndio chanzo kikubwa cha Dunia kutokuwa na amani either ni kwa kutokujua wao au kwa kujua vilevile, na yakawa yanafanyika makusudi kwa nia zao binafsi.\r\nTumeagizwa upendo kwa hiyo hatuna budi ya kuyachukia mataifa hayo,ila tuna takiwa kuongeza umakini ili tusije kuhatarisha taifa letu na watu wake.\r\nBinadam ni kiumbe dhaifu sana, na sio mwenye nguvu nyingi kama walivyo viumbe wengine kama walivyo wanyama wa kubwa na n.k.\r\nUdhaifu huu wa mwanadam ikapelekea apewe akili nyingi kuliko viumbe wengine kwa utashi na upendo wa mwenyezi MUNGU.\r\nKwahiyo mwanadam ni kiumbbe ambacho hakihitaji nguvu kubwa kukiua au kukiteketeza, maana kinaweza hata kufa peke yake chenyewe kwa sababu ya kukosa chakula kwa muda wa siku kadhaa. Vilevile mwenyezi MUNGU ambaye ndio muumbaji wake amesema, hakika hakitakuwa na siku nyingi za kuishi ni lazima kife baada ya muda wa miaka 70 au 80 kwa neema ya utii kwa mwenyezi MUNGU.\r\nMwanadamu ni kiumbe ambacho hakihitaji uwekezaji mkubwa, kwenye vitu ambavyo vinahitajika ili kumua au kuondoa uhai wake huyu mwanadamu. Kwa kuwa yeye ni kiumbe cha kawaida tu ambacho kinaweza kufa hata kwa kuchomwa na kisu au kitu chochote chenye icha kali.\r\nSasa kutokana na matumizi mabovu ya akili na maarifa aliyopewa huyu mwanadam, anatumia pesa au fedha nyingi kuwekeza kwenye masuala ya kutengeneza silaha mbalimbali kubwa za kivita. Kama vile nuclear, vifaru, mabom mbalimbali na magari ya kivita.\r\nUwekezaji huu ni mkubwa sana kwenye masuala ya kivita, na ni kitu ambacho hakikuwa cha muhimu sana kwa ajili ya usitawi wa Dunia na kudumisha amani. Uwekezaji wote huu wa silaha hizi za kivita sio kwa sababu ya wanyama wakali, ni kwa sababu ya mwanadamu, ambaye na uhakika hahitaji ndege kubwa au mabom na silaha kubwa za kivita ili kumwangamiza.\r\nIngewezekana tu kuwa na basitola au SMG kwa ajili ya kujilinda na wahalifu kama wezi na uhalifu mwingine. \r\nTechnologia ya masuala ya kivita ingekuwa imezuiliwa, ili kujiepusha na adha ya vitisho ambavyo vinamfanya mwanadamu aishi kwa wasiwasi na kuyaweka maisha yakemwenyewe kwenye hatari. Dunia ingeendelea kuwa sehemu salama na ya kupendeza kwenye kila pembe ya nchi utakayoenda.\r\nBajeti ya masuala ya kivita kote Duniani, ingetumika kutengeneza Dunia kuwa sehemu ya kuvutia na kujikita zaidi katika kutatua changamoto za kimazingira kwenye baadhi ya nchi.\r\nKwa mfano kuna nchi ambazo hazina chakula kutokana na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu, na kuandamwa na ukame wa mwaka hadi mwaka.\r\nBajeti hii ya masuala ya kivita ingeweza hata kutumika kwa kuhamisha au kujenga mitalo mikubwa ya maji, kutoka usawa wa maziwa au bahari kwenda sehemu yoyote ile ya nchi penye shida ya ukame na ukosefu wa maji.\r\nKwahiyo makosa yetu binadamu ya kutokutumia akili na maarifa yetu vizuri tuliyopewa na MUNGU, inatuweka kwenye shida hizi zote.\r\nMapinduzi na matumizi ya akili, ili kuleta mtazamo chanya kwenye jammii, na mabadiliko ya kweli kuanzia ngazi ya familia hadi Dunia nzima inawezekana. Kama tutachukua nia ya dhati ya kuyashinikiza mataifa makubwa yanayomiliki silaha na kuzitengeneza, tunaweza kufanikiwa angalau kwa kutengeneza mazingira mzuri ya kizazi cha watoto wetu watakao kuwa warithi wa nchi na Dunia kwa wakati wao.\r\nSasa tulikosea wapi? au tunaendelea kukosea sehemu gani? binafsi nafikiri watu wengi tunafeli hasa sisi tunaopiga kula, uwezo wa kumtambua kiongozi au uongozi ni nini kimantiki. Pia ufahamu mdogo wa kiongozi kuhusu uongozi wenyewe.\r\nNdugu zangu, UONGOZI au KIONGOZI ni kukubaliana na ushauri wa kila mtu, lakini kwa kuzingatia masilahi ya kila mtu. Kwa hiyo unaweza ukapinga au ukakubaliana na ushauri wa mtu kwa hoja za watu na kwa busara zako kama kiongozi.\r\nVilevile uongozi au kiongozi ni kuwa na uwezo mzuri wa kuwaelewa watu unaowaongoza, hapa viongozi wengi wameshindwa kuelewa kama sisi watawaliwa tunahitaji amani sio kutawaliwa. Ndio maana nchi nyingi duniani zinaingia kwenye matatizo ya kiutawala na kuwa chanzo cha vuguvugu la vita vya ndani kwa ndani.\r\nPia uongozi ni uwezo wa kuonyesha vitu kwa vitendo, kujitoa na kuyajua matatizo na changamoto za watu wengine. Kuathiliwa au kujisikia kuumia kwa dhati ya moyo wako kwa sababu ya watu wako unaowaongoza.\r\nUongozi ni kusimamia ukweli, ili haki ya mtu mwingine isije kupotea. Kuwa na maneno thabiti, usichanganye uongo kwenye maneno yako ili usije kuonekana mbaya, kwa sababu watu wanatunza maneno hasa ya viongozi na uongo husahaulika. \r\nSasa usije ukafanya watu wakatunza maneno ya uongo, hali ya kuwa wewe unaweza kuusahau uongo wako na ukaleta sintofaham badae.\r\nKiongozi sio mchoyo wa madaraka, anauwezo mzuri wa kutoa uongozi kwa mtu mwingine. Ili masilahi na haki za wale anaowaongoza zisipotee. Kiongozi anauwezo wa kutengeneza watu wengine kuwa viongozi bila kujali, na kwa kuzingatia sheria kama ni za nchi au jamii Fulani. Anaamini kuwa mafanikio yanaweza kuletwa na watu wengine pia, kwa msaada wake au kwa msaada wa wale anaowaongoza.\r\nKiongozi sio muonevu wala hana upendeleo, hafanyi vitu ili kuwaumiza watu wengine. Haibui vita ili kuonyesha au kuwaonyesha watu yeye ana nguvu ndio maana akawa kiongozi. Ni msitarabu na mtu anaethamini watu, hamwagi damu ya mtu kwa nia ya kujilinda. Kwa sababu yeye hulindwa na MUNGU kwahiyo hana hofu na mwanadamu. Ila huchukuwa tahadhali kwa ajili ya watu wake wasije kukosa haki zao.\r\nKiongozi anajiepusha na kuizuia migogoro isitokee, hatowi jeshi au silaha kukomesha au kutatua migogoro hata kukiwa na mgogoro mkubwa kiasi gani. Migogoro yote huifanya kuwa midogo na isilete madhara au athali kubwa, aidha kiuchumi au kijamii, nchi na nchi, taifa na taifa.\r\nMwisho kabisa kwenye suala la uongozi au kiongozi, uwezo wake unatakiwauende moja kwa moja kwa watu au jamii ya taifa lake anaowaongoza. \r\nUwezo wake uwe msaada wa kuwainua watu wake kiuchumi, au kwa kusababisha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii au taifa husika analoliongoza.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza