MAOMBI YA KUSHINDA VITA YA KIROHO
Kila jaribu Lina mlango wa kutokea, maombi yaliyopo kwenye kitabu hiki, yamebeba mlango wa kutoka kwenye changamoto zilizoshindikana.
Biblia inatuonesha kuwa maisha ni ya kiroho zaidi kuliko yalivyo ya kimwili, kwa sababu wakuu wawili wanaotawala maisha haya, yaani Mungu na shetani, sio wa mwilini bali ni wa rohoni.
Utawala wa Mungu katika maisha ya mtu utakuwa wenye nguvu zaidi, ikiwa mtu huyo atakuwa amejenga mahusiano bora na Mungu katika ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi na imani.
Utawala wa shetani kwenye maisha ya mtu utakuwa wenye nguvu zaidi, ikiwa mtu huyo atakuwa ameshindwa kumdhibiti shetani ipasavyo katika ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi ya imani.
Maombi yaliyopo kwenye kitabu hiki, yamevuviwa na Roho wa Mungu, ukiyaomba kwa Imani, utamdhibiti shetani ipasavyo, hivyo ushindi wako katika vita ya kiroho ni uhakika (Yakobo.4:7).
Chagua kifungu cha maombi kinachoendana na mahitaji yako, omba kwa imani, majibu ya ushindi katika maeneo yote ya maisha yako ni uhakika, wengi wameisha pokea majibu sasa ni wakati wako, wa kupokea muujiza wa MAOMBI.