MAMLUKI
Riwaya
MAMLUKI
Dunia ilishatangaziwa tanzia ya Pierre Businge. Dunia imekwishasahau jeuri ya Mo Mursal iliyotikisa viunga vya Mogadishu enzi hizo. Wawili hawa wanaibukia jijini Dar es Salaam, wakiletwa pamoja na dili ya kusafirisha kimagendo urani toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; dili wanayopewa na magaidi wenye uchu wa kuunda silaha za nyuklia.
Kati yao yupo Ayannah, msichana mrembo anayewatia wazimu wanaume hawa. Wako tayari kutoana roho juu yake lakini upepo unabadilika pale Pierre Businge aka Rish Kabasele anapokamatwa na kutupwa gerezani Butimba, akituhumiwa kwa mauaji na ujambazi. Bila Rish Kabasele dili imebuma.
Mwenye kuchinja hachelei kuchuna. Mo anafanya mchakato haramu kumtoa Rish gerezani. Kuifikisha uranium hiyo Bagamoyo mikononi mwa magaidi si jambo jepesi.
Kama mamba mawindoni, jasusi Patrice na Ian wanawafuatilia kwa makini, lengo ni kuwatia mbaroni magaidi na washirika wao, lakini siyo rahisi kihivyo!