MAMBO AMBAYO WANAWAKE WAZEE WAWAFUNDISHE WANAWAKE VIJANA
Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikifuatilia maisha ya wanawake vijana ambapo wengine ni marafiki wangu wa karibu sana. Nimepata nafsi ya kuzungumza nao mambo mengi na kujua maisha yao kwa ukaribu sana.rnrnBaada ya miaka mingi nimegundua tunaishi katika nyakati ambazo wanawake vijana waliowengi hawana na hawajui mambo ya msingi wanayotakiwa kuwa nayo ili waweze kuwa wake na mama bora katika familia zao.rnrnHali hii imesababishwa na kulelewa na kuzungukwa na wanawake wazee ambao nao hawana na hawajui mambo haya ya msingi, hata wale wanaojua wengi wao wameshindwa kuhakikisha wanawafundisha wanawake vijana ili wawe bora.rnrnKitabu hiki ni msaada kwa wanawake vijana kujifunza mambo ya msingi wanayotakiwa kuyajua na kuyaishi ili wawe wake na mama bora katika familia zao.rnrnLakini pia kitabu hiki kinawakumbusha wanawake wazee juu ya wajibu wao wa kuwafundisha wanawake vijana.rnrnJe? Unatamani kuwa mwanamke mzee bora na mwenye sifa za kuwafundisha wanawake vijana?rnrnUnatamani kuwa mke na mama bora katika familia yako?rnrn Jipatie nakala yako ya Ebook hii, utakapofika mwisho wa kitabu hiki utabadilika kabisa endapo utaruhusu maarifa haya kukubadilisha na kukujenga.