Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Mama Aminaaa - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali
Best Seller

MAMA AMINAAA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
3,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Oct 17, 2022
Product Views:
7,954
In category:
Sample

Story bora kuwahi kutokea.


MAMA AMINAAAAAAA

na @Mika Author

SEHEMU YA 01


Mama Amina ni mwanamke mjasiriamali katika mitaa ya buza jijini Dar.  Yeye kila siku usiku uwauzia watu supu na chapati. Ni biashara aliyoianza mara baada ya kuachwa na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni baba Amina. 


Alijitahidi sana kutafuta pesa kwaajili yake na mwanae,  Amina. Pesa ya chakula,  Ada,  Kodi ya nyumba na mengineyo lakini kadri siku zilivyosonga mbele ndivyo ugumu wa maisha ulizidi.  

Kutokana na ugumu wa fedha,  kila wiki Amina alirudishwa akidaiwa ada. Kwa kipindi hicho alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule  binafsi.  Matatizo ya ada yalizidi,  Amina alifukuzwa shule, na moja kwa moja akaachana na shule.


Baada ya Amina kufukuzwa shule, akaungana na Mama yake katika shughuli za uuzaji supu na chapati.  Mama na mwanae; kila siku jioni walielekea kijiwe maarufu cha boda boda,  wanywa kahawa, madereva bajaji n.k, huko ndiko walikesha hadi usiku wa manane wakisaka pesa.


Muda wao wa kurudi utegemea kuisha kwa supu. Siku supu ikiisha mapema,  walirudi mapema. Na siku supu ikichelewa kuisha basi waliisubiria. 


Huyo mama Amina huyo ukimuona ni balaa tupu! Kama ujuavyo mama ntilie wengi walivyo, mama Amina alikuwa kiboko yao. Hakuwa mnene wala mwembamba,  sio mfupi wala mrefu, mweusi wa kung'aa (black beauty) na huko nyuma sasa, wateja walipata shida. 


Labda sababu ya Maisha tu ndio maana aliangaika.  Lakini kuhusu uzuri;  alikuwa mwanamama mrembo. Mmama kama mdada! kila alikopita utasikia "Mama aminaaaa! "


Amina nae hakuwa nyuma.  Si unajua kuwa vya kurithi vinazidi? basi huyo Amina huyo, mtoto alikuwa na kishundu hadi sio poa. Kalikuwa ni kabinti ka miaka 16 lakini kila kanakopita utasikia "Aminaaa,  Aminaaa"


*******

Siku hiyo;  Ilikua ni usiku wa saa moja. Kama kawaida yake; Mama Amina na Amina wake walielekea kazini kwaajili ya shughuli yao. Waliweka majiko yao pembeni,  mkaa pembeni,  supu kwenye sufuria,  kindoo cha maji na vifaa vinginevyo.  Amina aliwasha moto,  supu iliwekwa jikoni ipate moto, jiko lingine walikaanga chapati. 


Taratibu wateja walianza kumiminika, bakuli moja 1000,  chapati moja 300. Watu walikunywa supu na chapati. 

Sio kwamba hakupata wateja,  wateja alipata. Sio kwamba hakupata pesa,  pesa alipata. Tatizo ni kwamba pesa alizozipata katika biashara hiyo hazikukidhi mahitaji ya familia. Supu na chapati pekee havikutosha kulipa kodi, kununua chakula,  mavazi na mengineyo. 


Licha ya mahangaiko,  alikuwa na misimamo.  Wateja wengi walinunua supu yake wakimvizia kimahusiano lakini walimkosa.  Kuna wateja wengine walimvizia Amina,  lakini mama mtu alikuwa makini. 


"Mama amina,  kwani we kwa siku unaingiza bei gani? "Aliuliza kijana flani ambaye ni dereva boda

"30,000 lakini faida 10,000" alijibu mama Amina

"Sasa sikikiliza.  Mimi nakupa 50,000 leo"

"Za nini? "

"Nipe mzigo.  Mara moja tu"

"Nani kakwambia najiuza? ebu niondokee kabla sijakuaibisha" alifoka 


(Dereva boda akaondoka kwa aibu)


Misimamo yake ilifanya baadhi ya wateja kupungua wakidai anaringa sana. Kitendo cha wateja kupungua kilisababisha mtaji wake kukata. Alianza kusuasua katika biashara,  leo alipika supu kesho hakuonekana! hali ilikua ngumu. 


Sio hivyo tu, mama mwenye nyumba Alidai kodi yake.  Tena ilikuwa kodi ya miezi mitatu ambayo alikaa pasipo kulipa. 


"Nakwambia kesho usipolipa unahama kwenye nyumba yangu" alifoka mama mwenye nyumba. 

"Kesho nitalipa"

"Ulipe utoe wapi?  We kila siku umekuwa wa kuomba msamaha tu. Ondoka ukapange sehemu nyingine"


Ilikuwa ni mshike mshike ndege tunduni.  Amina alitazama tu jinsi mama yake alivyoteseka. Kama mama alishindwa mtoto angefanyaje?  Ndio hivyo sasa.


Kelele za kodi zilimuumiza masikio mama Amina.  Aliamua kwenda kukopa pesa (20,000).  Yeye na mwanae waliamua kwenda kazini. Kama kawaida yao, majira ya saa moja usiku waliingia kijiweni.  Utata ulikuwa kwenye vazi alilovaa mama Amina. Usiku huo alivaa vazi jepesi mno. Alifanya vijana wa kijiweni wajazane wakimeza mate hovyo hovyo.  


Mama na mwanae waliangaika na supu hadi saa tano usiku. Licha ya supu kuwa chache lakini haikuisha.  Wateja walisusa kwa sababu muuzaji anabania mwili wake.  Hali hiyo ilimchanganya mama amina.


Mawazo ya kodi yalimjia,  alikumbuka pesa ya mkopo,  Pesa ya matumizi; kichwa kilimuuma. Masaa yalipotea,  watu walianza kuondoka pale kijiweni. Mama Amina aliogopa kurudi nyumbani! Mama wa watu plesha moyoni,  maumivu ya kichwa,  pia alihisi mkojo ukibana. 


Taratibu alipiga hatua kuelekea katika choo cha kike cha kulipia kilichopo pale kijiweni.  Aliingia na kujisaidia. Akiwa anarudi ghafla alidakwa mkono akavutwa pembeni.


Usikose sehemu ya pili


More Products On Discount
More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold
7,000 Tsh.

Sold by: Sadick Nzania

10,000 Tsh.

Sold by: Joseph Hoja

10,000 Tsh.

Sold by: LOUREEN JASPIN

10,000 Tsh.

Sold by: Sabra Amran

10,000 Tsh.

Sold by: Ezekiel Vigello