MALANGO YA MAFANIKIO YAKO KIBIASHARA
MALANGO YA MAFANIKIO YAKO KIBIASHARA
Ni shauku ya kila mfanya biashara kutimiza malengo yake ya kibiashara sawasawa na matamanio, mipango na ndoto yake ya kibiashara. Wengi hutamani sana lakini wasiweze kwa sababu hawajaitambua bado siri ya malango ya mafanikio ya kibiashara na ikiwa wanaijua basi hawajajitoa kuiishi ipasavyo au hawajajua umuhimu wake ili kupitia malango hayo waweze kufanikiwa kibiashara.
Mafanikio ninayoyazungumzia hapa ni ile hali ya mtu kufikia lengo lake au malengo yake ya kibiashara. Niliwahi kusema katika kitabu changu cha fanikiwa kuwa mafanikio ni kama nyumba na ili kutoka au kuingia ndani yake ni sharti mtu autambue mlango. Katika kitabu hiki ninaeleza baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa malango muhimu sana yatakayokuingiza kwenye mafanikio yako kibiashara.
Karibu tujifunze pamoja kwa kila neno, kwa kila sentensi na kwa kila aya. Utajuzwa mengi yatakayobadilisha hatima yako ya kibiashara na kukupa mtazamo mpya.