MALAIKA NI WATUMISHI WETU
Kitabu hiki cha Malaika ni Watumishi wetu, kimelenga kumsaidia kila msomaji na haswa jamii ya Wakristo na watu wote, ili kujua hakika ya uwepo wa Malaika na shughuli za Malaika. Watu wengi wamesikia habari za Malaika na wanajua kuwa Malaika ni kweli wapo, lakini wameshindwa kujua hao Malaika wanakazi gani na wapo kwa ajili gani. Tukija kwa sasa, wacha Mungu ndio kabisa, tumekuwa tukisoma katika maandiko kuhusu Malaika lakini hakuna anayejua kuhusu huduma za Malaika kwa wacha Mungu. Mathayo 4:11.... na tazama, wakaja malaika wakamtumikia. Hapo tumeona maandiko yakisema kuwa, Malaika waliweza kumuhudumia Yesu baada kumaliza mfungo wake wa siku 40. Hii ni wazi kabisa, sio kwa Bwana Yesu tu, bali ni kwa kila mtu aliyemuamini Mungu anayo haki ya kuhudumiwa na Malaika. Unapoendelea kusoma kitabu hiki, pia mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe zaidi katika huduma hii ya ajabu ya Malaika.
MALAIKA NI WATUMISHI WETU
Mamlaka na kazi za
Malaika
(a)
Mafanikio
Malaika ni mawakala wa
mafanikio, kwani na wao huleta kibali na baraka na maongezeko katika maisha ya
wanadamu.
Bwana, Mungu wa
mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi
niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka
malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko; (Mwanzo 24:7)
(b) Ulinzi
Malaika
ni mawakala wa Mungu kutupatia ulinzi. Na hivyo basi hutusaidia
kwenye vita vya kiroho pindi tu tunapoomba kwa Mungu na kuwaagiza huingilia
kati kutusaidia.
Malaika
wa Bwana hufanya kituo, na kuwazungukia wamchao na kuwaokoa
(Zaburi 34:7)
Kwa
kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao
watakuchuku, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Zaburi
91:11.12
Asiuache
mguu wako usogezwe; Asisinzie akulinde, Zaburi 121:3
Huduma
binafsi ya Malaika
Malaika hutuhudumia sisi
binafsi. Maelezo mengi katika Biblia huthibitisha kwamba, sisi watu huwa
tunashughulikiwa kibinafsi na Malaika. Mimi kama Mwinjilisiti, mara nyingi nimejiona kwamba sina nguvu za kutosha
katika viwanja vya mkutano, ili kusikia ujumbe kwa Bwana, lakini kila mara uchovu
wangu hutoweka na nguvu hunirudia tena. Nimekuwa nikijazwa nguvu za Mungu
katika nafsi yangu na mwili pia.
Kwa mfano: Eliya 1 Wafalme 19:4.7............Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili,
akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako.
Mara nyingi Mungu amekuwa
halisi kwangu. Akinitumia wageni wake wasioonekana. Yaani Malaika ili waniguse
mwili wangu wanifanye niwe mjumbe wake wa mbinguni. Ninene kama mtu afae kwa
watu wafao. Hatuwezi kugundua uwepo wa Malaika kila mara. Lakini Malaika huwa
jirani zetu. Mara nyingi wanaweza kuwa wenzi wetu pasipo sisi kugundua uwepo wao.
Tunajua mambo machache kuhusu huduma yao ya kila mara.
Hata hivyo Biblia
hutuhakikishia kwamba, siku moja macho yetu hayatakuwa tena na utando, nasi
tutaweza kuona na kujua upeo kamili wa huduma ambayo Malaika wametupa.
Nilipokuwa mtoto
mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri
kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya
kitoto. Maana
wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa
uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami
ninavyojuliwa sana.(1 Wakorintho 13:11.12)
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza