
MAKOSA UNAYOPASWA KUEPUKA UNAPOKUWA CHINI YA UONGOZI WA BABA WA KIROHO
Kama huna baba basi huna mabawa, huwezi kuruka ili kwenda mbali. Baraka za kiagano zinakuja kutokea kwenye agano la Mungu na baba yako wa kiroho, huwezi kuwa bora kuliko baba yako bali unaweza kuwa bora kwasababu ya baba yako. Kitabu hiki kimejikita katika kukusaidia kujua makosa unayopaswa kuepuka unapokuwa chini ya uongozi wa baba wa kiroho ili usikwame kiroho na kimaisha.
Maisha ya kiroho na maisha ya kimwili ya watu waliompa Yesu maisha yao yanauhusiano mkubwa sana na uwepo wa baba wa kiroho katika kuyafanya yainuke au katika kuyafanya yaharibike. Kulelewa chini ya uongozi wa baba wa kiroho kunahitaji nidhamu ya hali ya juu sana na gharama kubwa ili ikupe mlango wa kupata baraka za Mungu maishani mwako, vinginevyo unaweza kuambulia laana mbaya kutoka kwa Mungu na kukufanya ukwame na kuharibikiwa. Katika familia ya Nuhu, aliyekuwa baba wa kimwili kwa watoto wake lakini pia alikuwa baba wa kiroho kwa watoto wake kulikuwa na baraka lakini kulikuwa na laana. Ndiomaana Yuko aliyeambulia laana na wapo waliopata baraka kutoka kwa baba yao. Katika familia ya mzee Yakobo, kulikuwa na baraka lakini pia kulikuwa na laana, wapo waliopata laana na wapo watoto waliopata baraka. Matokeo ya laana yanatokana na baadhi ya makosa ambayo watoto wa kiroho wanaweza kuyafanya na wasijue Kama yanaweza kuwaletea laana maishani mwao na kusababisha kudumaa kiroho na kimaisha. Nimeona maisha ya watoto wengi wa kiroho yakiteketea kwasababu ya laana inayotokana na makosa wanayoyafanya kwa baba zao wa kiroho, na hii ndio sababu iliyoweka msukumo mkubwa moyoni mwangu wa kuandika kitabu hiki. Kuna jambo muhimu sana halijakaa sawa katika kanisa la leo, utaratibu wa makanisa mengi yameiua nafasi ya baba wa kiroho, na matokeo yake hakuna mpangilio wa Baraka za Mungu na utendaji wake katika kanisa. Adui amefanikiwa kuizuia neema ya Mungu iliyopo juu ya kiti cha ubaba isifanyike kuwa faida kwa wakristo! Wengine wamekataa kuitambua neema na nafasi ya ubaba katika kanisa, wengine wamekubali kuitambua lakini wanaendenda vibaya kiasi ambacho Baraka zilizokusudiwa kutoka kwenye mafuta ya ubaba hazilinufaishi kanisa na matokeo yake laana ya Mungu inalipiga kanisa na kuliharibu. Kinacholeta huzuni ni namna tuonavyo mababa wengi wanaondoka na neema walizopewa, maagano ya kiungu yaliyokusudiwa kusafiri vizazi na vizazi yanaishia kwenye kizazi kimoja cha maisha ya mababa katika ulimwengu kipindi cha uhai wao, na wakisha kufa wanaondoka na vitu vya kiungu kwasababu ya mkao wa kanisa lasasa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza