Makosa 6 Yanayofanywa Na Wasomi Wengi
Makosa 6 Yanayofanywa Na Wasomi Wengi ni kitabu ambacho kinakusaidia kujua makosa ambayo yamekuwa yakifanywa na wasomi wengi kabla na baada ya kumaliza chuo na jinsi ya kuyaepuka ili kufanikiwa maishani mwako.
Makosa 6 yanayofanywa na wasomi kabla na baada ya kumaliza chuo ni kitabu ambacho kinaelezea maisha yaw asomi kabla na baada ya kumaliza chuo.
Kitabu hiki ni tafakari na mwongozo wa msomi yeyotea mbaye yupo chuo na ambaye tayari kaishamaliza chuo.
Wasomi waliolengwa na kuelezewa ndani ya kitabu hiki ni wale ambao wapo au wamepita chuo kwa ngazi yaa stashahada mpaka udhamivu.
Kitabu hiki hakijaonyesha makosa tu, bali pia utatuzi wa makosa ambayo yamezoeleka lakini ndio chanzo pia cha hayo yote yanayotokea ndani ya jamii kwa wasomi kuonekana kama sio sehemu ya kutatua tatizo, bali kuongeza tatizo.
Vile vile ndani ya kitabu hiki mwandishi kaelezea dhamira yake ya dhati katika lugha ya kumlika giza kwa kutumia krunzi yenye mwanga mkali ili iwe rahisi kueleweka kwa wasomaji, hasa wale waliokusudiwa.
Makosa 6 yaliyoelezewa ndani ya kitabu hiki ni yale ambayo hufanywa na wasomi kabla hata ya kujiunga na chuo mpaka pale wanapomaliza chuo na kuingia mtaani au kurudi makwao. Kuna mambo ambayo mwanachuo alipaswa kuyafanya mapema hata kabla ya kufurahia tu kuwa kachaguliwa kujiunga chuo.
Kitabu hiki ni mwarobaini kwa wanachuo wote wanaoanza chuo bila kujua kuwa ni masomo gani ambayo wanapaswa kuyosomea kulingana na uwezo wao binafsi na sio kwa msukumo wa jamii na watu wanaowazunguka.
Kitabu hiki kisomwe hata kabla ya kuingia chuo kwa wale waliochaguliwa au wenye matarajio ya kuingia chuo kwasababu kinatoa muongozo dhahiri juu ya mambo ya kuyazingatia.
Kiufupi makosa ni mengi sana lakini ndani ya hiki kitabu mwandishi kaelezea makosa 6 ambayo kimsingi yameibuliwa na kujibiwa na mwandishi kupitia uzoefu wake na wa watu wengine ambao hata wao pia walishamaliza chuo na wale ambao bado wapo chuo.
Kitabu hiki kimetolewa kuwa mahususi kuonyesha, kuelezea, na kutatua changamoto mbali mbali zinazotokana na kuwa na ufahamu hafifu juu ya kipi kifanyike kabla na baada ya kumaliza chuo.
Makosa haya yapo, na bado yanaendelea kufanyika na ndio maana mwandishi akaona ni vyema kabisa kuandaa kitabu ambacho kitajibu maswali ya wengi na kutoa njia ambazo endapo zikitumiwa na kufuatwa ipasavyoi nakuwa sio rahisi kurudia makosa ambayo
yameshakwisha fanywa na wale ambao wameshamaliza chuo au kupita shuleni, hasa katika ngazi ya elimu ya juu.
Endelea kusoma zaidi…</>
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza