Makosa 4 Yanayofanywa Na 95% Ya Wauzaji Wa Bidhaa Za Afya
Ni kitabu kinachoelezea makosa 4 yanayofanywa na wauzaji wengi wa bidhaa za Afya na kuonesha suluhisho namna yakuweza kuyaepuka nakufanya mauzo yako kupanda zaidi kwa kujitofautisha na wauzaji wengine.rnrnPia utapata kuona mifano mingi juu ya namna gani uwe bora katika swala zima la uuzaji wa bidhaa hizo.
Najua unafahamu kwamba katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na kasi kubwa sana ya magonjwa yasiyo ambukizwa ambayo yamekuwa ni tishio kubwa sana duniani kote maana yanazidi kusababisha vifo vingi kila siku.
Kumekua na ongezeko kubwa sana la makampuni yanayojihusisha na uuzaji wa bidhaa za tiba lishe ikiwemo Ed mark international, BF Suma, Alliance in Global, Qnet na mengineyo.
Makumpuni yote hayo yameweza kutoa fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo kuweza kuwa msambazaji wa bidhaa zao.
Bila kusahau kuna watu binafsi wanaotoa huduma hizi kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.
Katika tafiti iliyofanyika chini ya Wabunifu Team Foundation juu ya Makosa yanayofanywa na wauzaji wa bidhaa za Afya ikaleta majibu na kubainisha wazi makosa mbalimbali ikiwemo, wengi kuuza bidhaa kwa 'mfumo huria' ikiwa na maana kwamba muuzaji unaingia sokoni na bidhaa yako bila kujua nani atakae nunua bidhaa yako na kwanini awe yeye na siyo mwingine.
Hapo muuzaji unataka kila mtu awe mteja wako, kumbuka hakuna mtu mwenye magonjwa kumi kwa wakati mmoja.
Hilo ni moja kati ya makosa ambayo yamefanyiwa tafiti nakuwekewa suluhisho ndani ya kitabu hiki ambacho kitakueleza makosa ambayo wewe kama mtoa huduma ya bidhaa za Afya haupaswi kuyafanya na suluhisho nyuma ya kila kosa.
Na pindi utakapo yabaini na kuyaacha nakuhakikishia mauzo yako yatapanda maradufu kwani utakuwa muuzaji wa kipekee na hautafanana na wauzaji wengi wanaotumia mbinu sawa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza