MAENEO MATATU YA KUSIMAMIA ILI MAISHA YAKO YAKAE SAWA
MAENEO MATATU YA KUSIMAMIA ILI MAISHA YAKO YAKAE SAWA
Kila unayemuona amefaninikiwa katika eneo lolote lile
basi ujue kuna maeneo matatu ambayo ameyasimamia
vizuri katika eneo hilo ambayo ni mwili, akili na roho.
Maisha yametutofautisha kwa zingatio la utofauti wa
viwango vyetu katika maeneo haya yaani namna
tunavyosimama na tunavyotumia fursa tulizonazo katika
maeneo haya. Ukitaka kuishi vizuri basi jitahidi kadiri
uwezavyo kuishi vizuri kwenye haya maeneo matatu
yaani mwili, akili na roho.
Luka 10:27, “Akajibu akasema, Mpende Bwana
Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na
jirani yako kama nafsi yako”
Maandiko haya yanaonyesha pia namna ambavyo
tunapaswa kuhakikisha tunakuwa vizuri na Mungu katika
maeneo haya matatu.
Kwa roho yako yote, mwanadamu ni roho ndani ya
mwili.
Kwa nguvu zako zote, mwanadamu ni mwili
Kwa akili zako zote, mwanadamu ana akili Basi nichukue fursa hii kukualika ili tuungane pamoja
katika kuzifunua kurasa za kitabu hiki ili tujifunze
kuhusu maeneo haya matatu ambayo ni muhimu sana
kwa uhai wa mtu katika kupelekea maisha ambayo ni
makamilifu na yaliyokaa sawa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza