Madhila
Madhila
Katika hii dunia binaadamu hupitia mitihani mingi sana, katika mitihani hiyo ni jambo la kupita tu. Hayo ndio majaribu ya maisha, hapo unaangaliwa utapasi au utafeli. Muhimu ni kuwa jasiri na kuchukulia majaribu hayo kama ni sehemu ya masomo yako katika hii dunia. Kuwa mvumilivu, jasiri na uzidi kumshukuru Mungu kwa neema nyingi alizokupa. Mitihani ni sehemu tu ya maisha yetu, kinachotakiwa ni kuzidi kumuomba Mungu atupe subira. Kumbuka neema alizokupa Mungu juu ya maisha, kisha ya akili pamoja na macho yako yenye uwezo wa kuona. Neema hazihesabiki alizotupatia Mungu, hata ukijaribu vipi maana ni nyingi mno. Madhila ya ulimwengu huu hayatokuacha, yatakuja na kuondoka, kitu kinachohuzunisha sana ni mtoto pale anapojiona yupo katika kituo cha kulelea watoto yatima. Hapo anakuwa yupo njia panda, hajui kama yeye ni yatima au wazazi wake wapo hai. Nini kilitokea hadi kuwa hapo kwenye kituo cha watoto yatima. Akiona wenzake shuleni wanataja baba, mama, dada au kaka. Hiyo inakuwa inampa maumivu makali ndani ya moyo wake.
Endelea...........!