Maarifa Ndani Ya Taarifa
Kitabu hiki ni maalum kwa watu wote wanaotaka kuona wanapata mabadiliko yanayotokea katika Karne hii ya 21
Maarifa ndani ya Taarifa ni kitabu chenye kuishi mahitaji ya karne ya 21. Waandishi Adv. Isaack Zake na Daniel Zake wanaeleza kwa ufasaha jinsi mtu yeyote anavyoweza kunufaika na taarifa zinazomzunguka kila siku.
Kitabu hiki kina Sura 4 ambazo zimejadili kwa kina juu ya Taarifa na Maarifa.
Sura ya 1
Maana, Makusudi na Chanzo cha Taarifa
Neno taarifa limefafanuliwa kwa undani sana kutoka asili ya neno hili kilatini 'informatio' . Pia imezungumzwa juu ya Makusudi ya Taarifa na Chanzo cha taarifa.
Sura ya 2
Kizazi cha Taarifa na Changamoto zake
Waandishi wanaeleza kwa ufasaha juu ya mabadiliko ya kitaarifa yanayoendelea kuhuhudiwa katika karne hii ya 21 inayotambuliwa kama 'information age' na namna wale wanaoujua ukweli huu wanavyoendelea kunufaika na mabadiliko haya huku wengine wasiojua wakiendelea kuwa watumwa katika zama hizi za taarifa.
Waandishi wanaeleza kwa mifano ya watu waliofanikiwa sana na kuwa matajiri wakubwa sana duniani kwa kujifunza kuitumia mifumo hii ya taarifa. Mfano ni Jeff Bezos wa Amazon, Bill Gates wa Microsoft, Mark Zuckerberg wa Facebook, Larry Page wa Google n.k. Halikadhalika wwandishi wameeleza athari hasi za mifumo mipya ya taarifa. Hii inampa msomaji fursa ya kufanya tathmini juu ya nafasi yake katika mifumo ya taarifa.
Sura ya 3
Nguvu ya Taarifa
Sura hii inaeleza kwa undani ni kwa jinsi gani mtu waathiriwa na taarifa anazopokea kila siku ziwe hasi au chanya. Hapa utajifunza juu ya mchakato wote wa taarifa ndani ya mtu kuanzia kupokea mpaka kuzitumia.
Sura ya 4
Waandishi wanaeleza kwa ufasaha katika sura hii namna msomaji anavyoweza kunufaika na taarifa kila siku. Hapa mikakati mbalimbali inajadiliwa kuhusu namna bora ya kuzitumia taarifa kutengeneza THAMANI katika jamii.
Waandishi wanahitimisha kwa kutoa ushauri wa makundi kadhaa ya wasiomaji namna ya kunufaika na kitabu hiki makundi hayo ni kama; Wanafunzi, Wazazi/walezi, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wasio na ajira na Watumiaji wengine wa mitandao.
Hiki ni kitabu muhimu sana kwa ajili yako, hakika utaona fursa mpya zinazokuzunguka kila siku kupitia taarifa na kubadilisha maisha yako na jamii kwa ujumla.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza