LINDA PENDO LAKO
MLINDE UMPENDAYE
Mara nyingi sana watu wamekuwa na bidii ya kutafuta wa kuwapenda na hii imepelekea baadhi ya watu kuhama kutoka mtu mmoja hadi mwingine wakidai kuwa yule aliye naye si sahihi au hajui kupenda. Naamini fika hata leo kuna baadhi ya ndoa zikivunjwa au watu wakipewa nafasi ya kuanza upya watu hawatataka kuoa au kuolewa na watu wale wale kwa hiyo wapo tu kwa sababu imeshatokea na wengine huendelea mbele tu kwa sababu wazazi wameshapokea mahali na kanisa walishatangaza hivyo hana jinsi zaidi ya kwenda kutumikia kifungo cha ndoa na si kuishi na kufurahia ndoa. Hii ni sawa na mtu anayehama kazi moja hadi nyingine kwa kigezo kuwa fedha anazopata hazikai/ hazitoshi.
Kitabu hiki kinawakumbusha watu wajibu ambao ni zaidi ya wajibu wa kutafuta na kupata na huu si mwingine ni wajibu wa kulindana na kuboreshana zaidi. Nakwambia unaweza kuwinda na kumpata mchumba uliyekuwa unamtaka na kumtamani sana awe mwenzi wako wa maisha lakini kama hujajua bado namna ya kulinda pendo lako itakugharimu na usipoangalia utajikuta ukiishi katika hali ya majuto kwa kudhani kuwa ulifanya uamzi ambao si sahihi kuoa au kuolewa na mtu huyo. Naamini kuwa ukikisoma kitabu hiki kwa makini na ukamruhusu roho mtakatifu akufundishe naamini hutabaki kama ulivyo na utakuwa na ndoa yenye furaha maana ndoa ndio hatma njema ya urafiki mzuri na uchumba wenye furaha.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza