KWELI ISIYOFUNDISWA KANISANI WALA MSIKITINI
Leo imekuwa Baraka na siku njema sana, machoni pa Mungu. Kama Mungu aishivyo iwe neema kwako wewe msomaji wa kitabu hiki, kuanzia leo na hata siku zako zote za maisha yako.rnrnNinapoandika ukweli kuhusu mafundisho ambayo hufundishwi kanisani au msikitini, sina maana ya kwamba yanayofundishwa kwa sasa sio mema. Na wala sio kwamba hayafundishi la! hasha, ila yako mafundisho mengi hayafundishwi kwa usawa au kwa usahihi ndani ya madhehebu tuliyonayo.rnrnPengine mafundisho haya, hayafundishwi aidha ni kwa kutokufahamu au ni kwa sababu ya masilahi ya kanisa. Inaweza kuwa, kwa sababu za kiimani nyingine kama vile uisilamu na imani zingine nyingi.rnrnKwa sababu Mungu wetu ni mmoja, na ni hakuna dini wale madhehebu yoyote yanayoweza kupinga ukweli kuhusu Mungu kuwa ni mmoja tu. Kwa maana hata wanaoabudu miungu mengine, wanajua kuwa kuna Mungu mmoja. rnrnMimi nina waandikia nyinyi na hata kizazi kijacho, kinachoamini kuwa mungu wetu ni mmoja.rnrnSina nia ya kubadilisha au kumbadilisha mtu imani yake, ila mtu atabadilisha imani yake baada ya kujua kweli ni ipi, kwa kuwa imani chanzo chake ni kusikia.rnrnNajua tunafahamu uwepo wa maagano mawili kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia, yaani agano la kale na agano jipya. rnrnSasa kabla hatujaendelea tuangalie kidogo kuhusu maana ya maagano haya mawili, na zaidi huko mbele tutajifunza kwa nini agano la kale na kwa nini agano jipya.rnAgano la kale, Agano la Kale ni jina ambalo Wakristo hupeana sehemu ya kwanza ya Biblia. Inakusanya seti ya vitabu vya kihistoria, vya unabii, hekima na mashairi ya dini ya Kiyahudi, pamoja na seti ya sheria za Musa.rnSehemu hii ya Biblia inakamilishwa na Agano jipya, ambalo linazunguka juu ya nafsi na mafundisho ya Yesu, na pia malezi na upanuzi wa wakristo. rnKwa mtazamo wa kikristo, Agano la kale linaelezea hadithi ya uumbaji na Agano jipya linaelezea historia ya wokovu.rnWakati Agano la kale, ni la kawaida kwa madhehebu yote ya ukristo, mkusanyiko uliokubaliwa na makanisa katoliki na Orthodox hutofautiana na mkusanyiko uliokubaliwa na waprotestanti.rnKanuni inayotumiwa na makanisa katoliki inafanana na ile inayoitwa Canon ya Alexandria au Toleo la sabini, iliyoandikwa kwa Kiyunani. rnrnKanuni ya sabini ina vitabu visivyotambuliwa na mila ya Kiprotestanti, ambayo ni: Tobias, Judith, Kitabu cha Makabayo, Kitabu cha II cha Wamakabayo, Hekima, Kikanisa na Baruc.rnKanuni ya Kiprotestanti inafanana na ile inayoitwa Canon ya Kiebrania au Kanoni ya Palestina, iliyoandikwa kwa Kiebrania, ambayo ina jumla ya vitabu 39 vya Agano la kale.rnMkusanyiko wote ulitumiwa kwa kubadilishana wakati wa Yesu, bila kuashiria tofauti kubwa za mafundisho kati ya Wayahudi wa kizazi hicho.rnKuna ushahidi kwamba, mitume walitumia toleo la sabini, kwa sababu theluthi mbili ya nukuu zao hurejelea vitabu ambavyo havikujumuishwa katika orodha ya Waebrania.rnSasa msingi wa agano la kale, ulitoka kwa mtu mmoja aliyeitwa Ibrahimu. Mungu alipomuita hakumuita ilimradi tu, bali aliingia agano naye akamwambia atambariki na kumfanya kuwa baba wa mataifa mengi, ikiwa tu atakuwa mkamilifu na atakwenda katika njia zake.rnMwanzo 17:1 “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. rnNami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. rnAbramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, rnMimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, rnwala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. rnNitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. rnAgano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. rnNami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. rnMungu akamwambia Ibrahimu, nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. rnHili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. rnMtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.rnUnaona, jinsi Mungu alivyokuwa mwaminifu, baadaye Mungu akaja kumtimizia kweli agano alilomuahidia, kwa jinsi uzao wake ulivyokuwa unaongezeka duniani kwa kasi.rnLakini wakati huo wote, uzao wake ulikuwa haumjui Mungu vizuri, ulikuwa bado haujajua kanuni za agano hilo, ambalo Mungu aliloingia na Ibrahimu baba yao linavyopaswa liwe.rnNdio hapo wakiwa kule jangwani, sasa Mungu anamtumia Musa kusema nao na kuwapa sheria na amri za kuzishika ili wafanikiwe.rnSheria hizo ndizo zilizoandikwa katika vitabu vya Torati: yaanirn• Mwanzorn• Kutokarn• Hesaburn• Mambo ya Walawirn• Kumbukumbu la ToratirnHivyo vitabu vitano vilikamilisha sheria yote ya Agano hilo, ambalo Mungu aliingia na Ibrahimu.rnLakini hiyo peke yake haikuwa inatosha kwa wana wa Israel kumfahamu Mungu katika ukamilifu wote, Hivyo ilipasa Mungu azungumze nao mara kwa mara kupitia watu mbalimbali wakamilifu na manabii wake. rnMfano tunamwona mtu kama Ayubu, Esta, Ruthu, kwa kupitia maisha ya hawa Mungu aliwafundisha wana wa Israel jinsi ya kuishi katika njia zake. rnVilevile akawa anasema nao mara kwa mara kupitia manabii wake wengi, na waamuzi mfano Samweli, Isaya, Yeremia, Danieli, Yona, Malaki na wengine wengi tu Biblia imeweka wazi.rnHivyo kwa kupitia hao pia, na vitabu vyao walivyoviandika, iliwasaidia wana wa Israel walishike na kulikumbuka agano ambalo Mungu aliingia nao zamani.rnKwahiyo tunapovisoma vitabu 39 vya Agano la kale, tunafahamu kuwa ni jumuisho la sheria zote na kanuni zote za Mungu kwa wale alioingia nao agano kupitia Ibrahimu.rnSasa mpaka hapo nafikiri utakuwa umeshapata msingi wa Agano la kale kwa ufupi, lilipoanzia na sababu ya agano hili kuwepo.rnAgano jipya, Hili nalo Mungu aliingia katika agano na mtu mmoja tu, kama vile alivyoingia na Ibrahimu. Na mtu huyo sio mwingine zaidi ya YESU KRISTO.rnIbrahimu alipewa tu uzao wake wa kimwili, lakini huyu alipewa uzao wa wote wenye mwili wakimwamini tu kwa kuzaliwa mara ya pili.rnNa ndio maana kuna umuhimu wa kila mmoja wetu kuzaliwa mara ya pili, ili tufanyike kuwa uzao wake, yeye mwenyewe alisema.rnYohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.rnNa kubatizwa kwetu ndio ishara ya tohara yenyewe ya rohoni, kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu na watoto wake wote, walipotahiriwa kwa kutolewa magovi. rnVivyo hivyo na sisi tunapaswa kubatizwa, kama ishara ya kutahiriwa mioyo yetu. Maana hatuko chini wale hatuongozwi na ile sheria tena, kwa sababu ya ondoleo la dhambi alilolifanya Yesu KRISTO.rnLakini tukishazaliwa mara ya pili, hilo tu peke yake halitoshi, ni sharti pia tujue kanuni, na amri za Mungu anazozitaka za agano hili, ili tuweze kudumu ndani yake. rnKama uzao wa Ibrahimu ulivyopewa kanuni na sheria za kufanya, ili wawe wakamilifu mbele za Mungu.rnHapo ndipo vitabu vya Injili ya Yesu Kristo, na vile vya mitume, viliandikwa kwa ajili yetu ili sisi sote tutakapovisoma na kuvishika, basi tuweze kudumu na kuimarika katika hilo agano jipya la Damu ya Yesu Kristo.rnNdipo hapo tunakutana na vitabu 27 vya agano jipya.rnHivyo kwa hitimisho fupi, Agano jipya ni agano Mungu aliloingia na Yesu pamoja na uzao wake wote. Ambao mimi na wewe tunahesabiwa katika uzao huo, kwa kumwamini Yesu na kubatizwa.rnTukifanikiwa kufanya hivyo, basi baraka zote Mungu alizomuahidia Yesu Kristo, na sisi sote pia tunazishiriki na kuzirithi, ikiwemo uzima wa milele.rnKusudi la kitabu hiki, ni kukufundisha vitu ambavyo inaweza kuwa ni mara chache sana, kwa viongozi wetu wa kidini na kiimani kutufundisha.rnKwa ajili ya uoga wa kuligawa kanisa, au kuleta mapungufu kwa imani tulizozipokea zamani.rnNalejea kusema kwamba kitabu hiki hakilengi kumtoa mtu kwenye imani yake, ila kitakufanya ufahamu ni mahali gani uliposimama. rnJua urithi wako uliyoupoteza miaka mingi tangu enzi za mababu.rnNaomba Roho mtakatifu akuongoze katika kuelewa, kwa maana naandika kitabu hiki kwa uthibitisho mwingi kutoka kwenye vitabu vyetu mbalimbali vya dini.
<!--[if gte mso 9]><xml>rn
YALIYOMO
rnrnrnrn
rnrn
rn rn | rn rn SHUKRANI rn | rn rn i rn | rn
rn 1 rn | rn rn UTANGULIZI rn | rn rn 1 rn | rn
rn 2 rn | rn rn KOSArn LA KUKUBALI rn | rn rn 11 rn | rn
rn 3 rn | rn rn BAADHIrn YA MAKOSA YALIYOMO KWENYE BIBLIA TAKATIFU rn | rn rn 29 rn | rn
rn 4 rn | rn rn JE!rn LAANA YA HAMU NI CHIMBUKO LA WATU WEUSI rn | rn rn 46 rn | rn
rn 5 rn | rn rn UBATIZOrn SIO WA MAJI MENGI WALA MACHACHE rn | rn rn 53 rn | rn
rn 6 rn | rn rn MASOMOrn NANE YA KUJENGA IMANI YAKO rni. rn Somorn la kwanza…………....….78 rnii. rn Somorn la pili……………………86 rniii. rn Somorn la tatu……………….…..97 rniv. rn Somorn la nne…………..……...101 rni. rn Ninirn uzima wa milele…112 rnii. rn Mbingunirn ni wapi….....122 rnv. rn Somorn la tano………...…….....129 rnvi. rn Somorn la sita…………..….…...142 rnvii. rn Somorn la saba………………….148 rni. rn Kiyamarn ya kwanza…..151 rnii. rn Kiyamarn ya mwisho…..153 rnviii. rn Somorn la nane……………...….158 rn | rn rn 78 rnrn rn rn | rn
rn 7 rn | rn rn INJILIrn YA NICODEMUS rni. rn Surarn ya I………………..……...166 rnii. rn Surarn ya II…………….......…..172 rniii. rn Surarn ya III………………….…176 rniv. rn Surarn ya IV………………….…178 rnv. rn Surarn ya V……………………..181 rnvi. rn Surarn ya VI………………….…188 rnvii. rn Surarn ya VII…………………...192 rnviii. rn Surarn ya VIII…………………..194 rnix. rn Surarn ya IX………………….…197 rnx. rn Surarn ya X………………….….205 rnxi. rn Surarn ya XI……………………210 rnxii. rn Surarn ya XII…………………...215 rnxiii. rn Surarn ya XIII……………....…..218 rnxiv. rn Surarn ya XIV………....………..220 rnxv. rn Surarn ya XV…………….……..224 rnxvi. rn Surarn ya XVI…………….……..228 rnxvii. rn Surarn ya XVII………………..…231 rnxviii. rn Surarn ya XVIII………………...234 rnxix. rn Surarn ya XIX…………………..237 rnxx. rn Surarn ya XX…………………...240 rnxxi. rn Surarn ya XXI………………..…243 rn | rn rn 163 rn | rn
rn 8 rn9 rn | rn rn YESU,rn MADHEHEBU NA DINI rnUHURU,rn NEEMA NA TORATI rn | rn rn 248 rn266 rn | rn